OMBI: Serikali idhibiti bei kwenye vifaa vya kujikinga na kupambana dhidi ya Virusi vya Corona

OMBI: Serikali idhibiti bei kwenye vifaa vya kujikinga na kupambana dhidi ya Virusi vya Corona

Umesema jambo la maana Sana mkuu, lakini nasikitika kuwa hilo lazima litokee kwasababu

Kwanza udhibiti utakuwa mdogo kwasababu serikali itatumia nguvu kubwa kwenye kupambana na corona hivyo upande huu unaweza kusahaulika.

Pili ni shortage ya bidhaa iyaweza kutokea kutokana na kukwama kwa biashara hasa international trade, kumbuka tunategemea bidhaa nyingi kutoka nje. Ikitokea mipaka ikafungwa biashara itaathirika na hivyo kupelekea upungufu wa bishaa na hapo mfumuko wa bei utatokea.

Tuombe Mungu madhara ya Corona yasiwe makubwa ili tusifike huko.
 
Dam55,
Itabidi wauze kwa bei walizonunulia mwanzo kabla ya janga kutokea katika bei ya pili watasubiria ushauri na maelekezo kutoka serikalini iwapo bidhaa zinapatikana nje ya nchi au hazipatikani tena
 
Idd Ninga,
Wanachofanya sasa ni kuzifanya hizo bidhaa ziadimike! Nimetoka muda mfupi tu kutafuta sanitizer na mask kwenye pharmacy kubwa hapa mjini na wameniambia zimekwisha! Sasa sijui kama zimekwisha au wanasubiri mpaka watu tuanze kuhaha ndio watupige na bei za kunyonga! Kweli aliyesema kufa kufaana aliwaza sana aiseeh!
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana janga kama hili unakuta MTU ndiyo anataka atajirike....huu ni unyama,Jana jamaa YANGU kaenda huko posta DSM anataka kununua box LA musk hizi za kujikinga kuuliza bei anaambiwa kwa sasa musk moja inauzwa shilingi 8000/=,wakati mwanzo ziliuzwa 500/= yaani ni shida sana hapa ubinaadamu hakuna kabisa.

Unapandisha bei ya bidhaa wakati hilo janga linaweza likakutafuna hiyo faida kubwa sijui utailia akhera,serikali iweke mkazo kwenye hili LA sivyo itakuwa ni maafa ya kutisha.
Huwa wanasema kufa kufaana
 
Bora hata nyie mna pesa za kununulia masks wengine hata ela ya kula ni mtihani sembuse hizo mask na mazaga mengine...we kama una nafasi ya kununua nunua tu mkuu hakuna namna maana yajayo yana furahisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
naona serikali wametekeleza ombi langu.
 
Corona imekua gumzo kona zote za nchi. Kila mtu amejawa na hofu juu ya hivi virusi vinavyosambaa kwa kasi kila kona ya dunia.

Kila mtu anatumia uwezo alionao kuweza kujikinga na virusi hivi. Moja kati ya hatua za kuchukua tahadhari ni kuwa na vimiminika vyenye uwezo wa kuua bakteria.
Hapa naongelea sanitizer na spirit.

Imekua kawaida kwa kila changamoto kufanywa fursa kwa wenye macho na uwezo wa kuwaza haraka. Hakika huu ni wakati wa wenye PHARMACY. Sanitizer na spirit vimegeuka kuwa bidhaa adimu baada ya kila taasisi, kampuni, mashirika na watu binafsi kutaka kujikinga na virusi hivi.

Jana asubuhi lita moja ya spirit ilikua shilingi 5,000. Mpaka muda huu naongea spirit lita moja inauzwa kwa shilingi 20,000.
Sijui kwa kesho itafikia bei gani.

Kwa hili ningependa serikali iliangalie kwa jicho la ndani maana watu wa hali ya chini hawataweza kumudu bei hizi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyabiashara wenye uchu wa kupata faida kubwa sasa wamegeukia fursa ya Corona kwa kuuza sanitizer na mask kwa bei ya juu.

Jana nimefika kwenye duka fulani nikaulizia bei ya sanitizer wakaniambia ni kuanzia Tshs. 45,000 mpaka 50,000 na bei ya mask ni Tshs. 5,000.

Ninaishauri Serikali kama kweli wanawapenda wananchi wake vifaa hivi vipelekwe hadi kwenye Mamlaka ya Kitongoji au Mitaa ili wananchi aidha wauziwe kwa bei nafuu au wapewe bure.
 
Serikali, igawe bure, ili kulinda jasho la mlipa kodi; lisipotee bure!
 
Hizo mask mnavaa za nini? Mbona mnakuwa wajinga sana!

Yaani sijui ni ulimbukeni? au ni ujinga tu uliosababishwa na madhara ya shule za kata!?

Hakuna mtu anayehitaji kuvaa mask! Just be clean and wash your hands with water! Inatosha.
 
Idd Ninga,
Wanachofanya sasa ni kuzifanya hizo bidhaa ziadimike! Nimetoka muda mfupi tu kutafuta sanitizer na mask kwenye pharmacy kubwa hapa mjini na wameniambia zimekwisha! Sasa sijui kama zimekwisha au wanasubiri mpaka watu tuanze kuhaha ndio watupige na bei za kunyonga! Kweli aliyesema kufa kufaana aliwaza sana aiseeh!
Leo nimerudi hizo pharmacy! Unajua wanauzaje mask iliyokuwa inauzwa kwa 600-1000/=! Inauzwa 3000/= (buku tatu(zaidi ya x3 ya bei ya awali) Box lenye mask 100 lililokuwa kinauzwa elfu 50, ni sawa kwa sasa na laki tatu!
 
Leo Ktk pitapita zangu nikitafuta vitu vya kujikinga, nimepitia pharmacy kadhaa kubwakubwa ambazo juzi nilipopita walinieleza kuwa masks na sanitizer zilikuwa zimeisha pharmacy!

Unajua wanauzaje mask iliyokuwa inauzwa kwa 600-1000/=! Inauzwa 3000/= (buku tatu(zaidi ya x3 ya bei ya awali) Box lenye mask 100 lililokuwa linauzwa elfu 50, kwa sasa ni laki tatu! Kama kwa box moja lenye mask 100 walipata faida ya 10,000/= mpaka 100'000/=,

leo ni 250,000/= faida kwa rejareja! Kumbuka hizi mask za kuvaa mara moja na kutupa(huvai zaidi ya masaa 3 bila kubadili nyingine mpya, na wala hazifuliki(sio za kuvua) Huu kwa kweli ni ujambazi wa mchana kweupe!
 
Hakuna Sababu ya Kuvaa Mask unless umeshapata maambukuzi...Ambapo unatakiwa uwe kwenye Quarantine...

Njia nzuri ya kujikinga ambayo Ni effective na haiitaji gharama zisizo za lazima Ni kunawa mikono kwa maji na sabuni, na kuepuka kujishika usoni..

Hakuna namna kutakuwa na demand kubwa ya bidhaa fulani na Bei isipande..Hata Nyanya zilipanda Bei..

Hofu Ni kubwa kuliko Corona yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kulalamika umeisha ambiwa na watahalamu mask ni muhimu sana kwa mgonjwa na kwa anaemuhudumia mgonjwa
Iyo sanitizer ya mikono ukiacha ya ambayo iko kwa mask kweli kwa sasa Nazo zimepanda ila kwa tusiojua sanitizer hasa za kunawa mikono ni kingereza tu but spirit tuwekayo may be bahada ya kunyoa nywele bado ni senitizer nzuri,wasiwapige kwa kingereza cha senitizer spirit bado ni kitu kile kile tu wamebadilisha neno hakuna jipya hapo
 
Nyinyi wakulima mlikuwa mnatuambie kama chakula gharama tukalime.

Sasa ni zamu yenu pia, kama hamuwezi nunua katengenezeni zenu. Nguo si mnazo nyumbani.

Dah,...nilikosa hamu kwa majibu haya. Acha tupambane tu,korona atoweke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom