Kumekuwepo na upandaji wa bei za barakoa ambazo ukiangalia ni za aina moja. Bei nilizosikia ni kuanzia 53,000 na wengine wanatangaza bidhaa ile ile kwa TZS90,000 na yawezekana kuna wanaopandisha zaidi.Na nahisi hata hiyo 53,000 ni bei ya juu.
Suala la kujikinga lisiangaliwe kibiashara zaidi, hapa tunaokoa maisha yetu na nchi kwa ujumla, hivyo bei za hizi bidhaa ingekuwa vyema kama mamlaka husika wangeweka bei elekezi ili watu wengi waweze kumudu kuzinunua na kuzuia upandaji wa bei huu tunaouona.
Hii ni vita yetu sote, kipindi hiki hela pia ni ngumu maana biashara nyingi zinafungwa. Hivyo mamlaka zisaidie hizi barakoa zenye ubora zipatikane kwa wingi ila kwa bei ambayo haiumizi watu. Kama mtu anaweza kuuza kitu kile kile kwa 50,000 na mwingine 90,000 ina maana kuna kitu hakipo sawa.