Ommy Dimpoz amkana baba yake

Ommy Dimpoz amkana baba yake

Niliwahi kukutana na huyu Mzee Sumbawanga ni dereva Bajaj.

Wakati napata huduma ya usafiri wake alikuwa analalamika sana juu ya Ommy na kubwa zaidi akisema suala lake na mwanae limesababishwa na Mama yake Ommy.

Inaonekana wakati huyu mzee akiwa kijana hakuwa karibu na familia yake kihivyo.

Bajaj yake imeiandika "Pozi kwa Pozi"
 
Tatizo la wazazi wanashirikisha watoto na kuwajaza sumu
Hapo mtoto lazima aende kwa baba na kutafuta ukweli huku akijua atakutana na maneno ya ukweli kuhusu mama yake


Wengi wa kina mama huwa wanajikosha kwa watoto pindi wanapovuruga ndoa zao (sio wote)
Unakuta mama anaongea na watoto na kusema baba kawatupa kumbe yeye ndio alichepuka, Baba kuona hivyo kakimbia kwa aibu ila kesi inamuangukia yeye

Kana mama mbona hamsemi ukweli yanapotokea ya kutokea?
Inaweza kuwa sababu nyingi nyingine ila kuachana au mmoja kuondoka lazima kuwepo na kitu kilichomsukuma kuondoka nyumbani
Ila watoto mnapokuwa waulizeni wazazi ukweli badala ya kumkataa mzazi kisa umepata maisha mazuri

Na wazee waache kujipendekeza au kulalamika bali waseme ukweli mtupu hata kama ni mchungu
 
Ya Ngoswe.... kuna Ommy Dimpoz, kuna Mond... na kuna Tupac
Msikie Tupac nae alivochefukwa kwenye DEAR MAMA na wala hakuficha hasira zake kwa Babake:
"No love from my daddy, 'cause the coward wasn't there
He passed away and I didn't cry, 'cause my anger
Wouldn't let me feel for a stranger
They say I'm wrong and I'm heartless, but all along

I was lookin' for a father, he was gone...
Soma kwa makini hiyo mistari miwili niliyoBold.... ndicho kinachomsibu Ommy Dimpoz
Kaamua kuishi maisha ya kipekee
 
Kweli sijawahi kuskia mtoto akimkataa Baba tajiri kwa madai kwamba alimtelekeza mama yake, Lakini watoto wakitajirika wanawakataa Baba maskini kwa kigezo cha Utelekezwaji.
Hii ni direct imbalacement.

Na Mimi sijawahi kusikia mzazi akaenda kumng'ang'ania ubaba au umama kwa mtoto teja

Ommy mama yake kafariki akiwa la pili huko, ina maana hizo sumu alilishwa wapi

Kama alimtafuta mzee na kumpata na bado akaonesha kwamba watoto aliozaa nje kwake ni extra tu, ulitaka jamaa afanyaje

Nina wasiwasi kama hata umelelewa malezi ya single parenting let alone kumuona hata mtu wako wa karibu kapitia. Ungefuta haya maneno
 
Issue ni kuzaa si kulea, Baba na Mama ni wale wanaokuzaa. Unaweza ukalelewa hata mituo cha polisi na Maaskali lakini huwez kuwataja kama Baba na Mama yako
Kwani kuzaa kuna nguvu gani inatumika special

Si ni ile ile tu ambayo watu hutumia kufanya mapenzi na makahaba na sperms kutupwa chooni

Bhana uzazi ni kulea,

mtu anaehangaika usiku kucha ukiumwa,

Mtu anaepigania future yako, usome na ile vizuri, mtu anaekuwepo kwenye moments zote, huyo ndio mzazi maana hakuna bond inayoundwa pasipo matendo

Kama huyo mzee angeonesha excitement ya kumiss moments na mwanae ningesema ommy ana makosa

Mtu kakutafuta lakini bado hujaona umuhimu wa kuwa nae karibu, Leo kafanikiwa ndio unamuona mtamu. Asee Mimi simlaumu jamaa, asiforce vitu kufurahisha raia kama moyo wake haujaridhia
 
Sema watu utazama zaidi negativity, hivi kwa mfano mzazi alikutelekeza then ukalazimika ukapambana na hadi ukatoboa kwa hasira, Mimi binafsi kama positive man lazima nikurespect mzazi kwamba kunitelekeza kwako ndipo kumenifanya nifanikiwe, maana ungenilea vyema nisingekaza ningekuwa labda bodaboda, dereva au muajiriwa fulani masikini hivi.
So dimpos, diamond, Elon musk, luck dube wawashukuru baba zao kutokuwa karibu nao kumewafanya watoboe.
Kwahio watu waliolelewa na wazazi wote wawili ni masikini?
 
Kuna mambo mengine wanawake wanayatengeneza wenyewe mimi mwanangu sijawahi hata mgusa zaidi ya kupewa picha mbili tatu tena kwa mbinde sana, mama yake ni kiburi tuu kimemjaa kisa kwao uwezo upo mtu anakaa kibaha anataka kuandikisha clinic lugalo nikahoji huko kibaha hakuna hospitali??

Akajibu ooh kugalo hospitali tunayoitumia familia nikamwambia huoni kwamba utajitesa na mambo ya nauli akadai atapelekwa na mamaake mdogo usafiri upo nikatulia nisikilizie siku ya clinic sasa anataka nauli sijui sasa hapo nilimpaga hela ya vifaa ili akiamua kwenda mambo yakae sawa siku ya kwenda anataka nauli hela ya clinic vifaa ile anadai alikula so jumla 270k kila kitu nikamwambia sina hela iyo nilichukia sana.

Ila ni kama ilikuwa sababu akaniambia namchukulia kama ana njaa sana basi nitulize nione kama ataniomba tena, akanilia buyu nikajua labda hasira za mimba mwee ndo ikawa ntolee iyo..nikimwambia nikutumie hela za kujikimu anadai Bi mkubwa wake kashalipa hana shida mapaka anajifungua ni kuchuniwa.. mwenyewe nikaona nibalansi shobo tu..
Hata mm ningekufungia vioo...
 
Na Mimi sijawahi kusikia mzazi akaenda kumng'ang'ania ubaba au umama kwa mtoto teja

Ommy mama yake kafariki akiwa la pili huko, ina maana hizo sumu alilishwa wapi

Kama alimtafuta mzee na kumpata na bado akaonesha kwamba watoto aliozaa nje kwake ni extra tu, ulitaka jamaa afanyaje

Nina wasiwasi kama hata umelelewa malezi ya single parenting let alone kumuona hata mtu wako wa karibu kapitia. Ungefuta haya maneno
Mtu anashupaza shingo kuwa Ommy kalishwa sumu huku mama mwenyewe alifariki wakati mtoto ni mdogo. Wengi wanaongea tu hawawahi kuwa kwenye situation kama za Ommy.
 
Back
Top Bottom