Naunga mkono hoja, Kwa vile ziara za ughaibuni bado ni nyingi zinakuja, September mwishoni na October Mwanzoni Mama anakuja tena US kwenye UNGA, sisi akina kajambanani, washauri wa bure wa huku mitandaoni, tutamshauri, hana sababu ya kuogopa lolote. Tutamshauri aige baadhi ya tabia nzuri za JK na JPM, kwenye ziara, likitokea jambo ambalo halimo kwenye ratiba, avunje ratiba aliruhusu.
Na wana diaspora wa upinzani, kama mna hoja za kweli na mna nia ya maandamano, pangeni maandamano rasmi, ujulisheni ubalozi, onyesheni mabango neat, sio ule uchafu, kuweni na wasemaji rasmi, fanyeni uhamasishaji, Mama hana problem yoyote kuwaona, kama amenikaribisha Mbowe Ikulu, what about you?. Japo rais ni kiongozi wetu mkubwa, ni mtumishi wetu, sisi Wananchi wa Tanzania ndio mabosi wake, tuliomuajiri kwa kura zetu na tunaomlipa mshahara kwa kodi zetu hivyo lazima atusikilize.
P