Kaka ujumbe wangu ni ule ule punguza jazba wakati unaongea na watu ambao huwajui vizuri. Nilijenga hoja ya kukwambia mimi sio mtutsi nikakupa historia ya wazazi wangu kwa ufupi tu. Wewe unakuja humu JF unajifanya unajua mambo ambayo kwa maandishi yako jinsi yalivyo, inaonyesha umesikiliza story za wakubwa zako, na story zenyewe unazileta humu zikiwa na makosa mengi ya details. Unadanganywa na watu kuhusu Kagame na wewe unaingia kichwa kichwa. Points zangu zinabakia pale pale kwamba mentality za kitanzania lazima zibadilike ikiwa tunataka kufika mbali. Kama moyo wako umeumia kwa sababu Kagame kapewa sifa anazostahili, sina cha kufanya kwa ajili ya kukuponya. Kagame licha ya madhambi yake mengi, bado ameweza kufanya vitu vingi wakati sisi tukiwa tumekwamba kwenye majibizano mengi ya wanasiasa. Tanzania yetu kila mtu anajua kila kitu, very wrong concept.
Filipo
Jambo usilo lijua ni kama usiku wa kiza.
Ni vyema ungenyamaza na kujifunza wanayo andika wajuvi.
Huwezi kuitwa mjinga wala mpumbavu kwa kutokujua.
Kwa haraka nimegundua wewe ni mtu wa aina gani.
Usilazimishe, weka sikio lako chini utafaidika dogo.
Hao Rwandese-Tutsi tumewaoa na kujukuu nao
Tunawafahamu, Tunawajua kinaga ubaga.