Salaam wana MMU
Ambao hamjaoa usipite bila kusoma huu uzi.
Wahenga walisema kuishi kwingi kuona mengi. Pia tembea ujionee. Misemo hii katu usije ukaipuuza hasa linapokuja suala la kupata mwenza wa maisha.
Kwa kipindi kirefu toka nimalize masomo, nilijikuta nimenaswa kwenye kazi za kitumwa hizi as desk officer mjini, 24/7 unashughulika na matatizo ya watz yasiyoisha.
Mwishoni mwa mwaka Jana Kuna fursa ilijitokeza , nikapewa kuwa sehemu ya timu itakayotekeleza kazi hiyo mikoa kadhaa nchini, mjini na vijijini.
Exposure kubwa niliyokua nayo ni maisha ya mjini yaliyojas stress. Kila mtu kavurugwa na maisha na watu wamekaa kipigaji tu. Unakuta hata wapenzi wanaishi Kwa kuliana timing , ukizubaa unaopigwa tukio.
Kwa miezi michache nimekaa vijijini na miji midogo ukanda wa kati. Kuna exposure mpya nimepata hasa Kwa mabinti na wanawake wa kitanzania. Unakutana na mabinti wazuri , natural beauty, ukiongea nao wana maisha magumu sana, ila uzuri wao umefichwa kwenye tamaduni za kijijini. Cha ajabu wana mitazamo Chanya, na wala ugumu wa maisha haujafanikiwa kuondoa tabasamu lao.
Nilichojifunza, usifanye uamuzi wa kuoa kama hujatembea nje ya eneo lako . Toka nje, zunguka mikoa kadhaa, explore, utakutana na dhahabu ambazo ukiziosha, zitatoa nuru.
Kijana pokea salaam hizi kutoka Kwa mtembezi. Usiache kuzifanyia kazi. Wasalaam.