HOJA Ongezeko la Excise Duty kwenye magari ni changamoto mpya kwa Wananchi

HOJA Ongezeko la Excise Duty kwenye magari ni changamoto mpya kwa Wananchi

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Wizara ya Fedha imewasilisha bajeti ya mwaka mpya ambayo imejumuisha ongezeko la kodi ya excise duty kwa magari, ambapo baadhi ya magari yameongezewa kwa asilimia 10 na mengine kwa asilimia 5 kulingana na umri wa gari.

Sisi wafanyabiashara tunaelewa kuwa kodi ni wajibu wetu na hatupingi kulipa. Hata hivyo, tunaiomba Serikali kutoa angalau kipindi cha mpito cha siku 30 kabla ya kuanza kutekeleza mabadiliko hayo, ili wafanyabiashara ambao tayari walikuwa wameagiza magari kutoka nje waweze kujipanga.

Mfano mzuri ulionekana wakati Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilipoongeza tozo ya PID na kutoa kipindi cha mpito (grace period) kabla ya kuanza utekelezaji. Tunahoji kwa nini utaratibu kama huo usitumike pia kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wizara ya Fedha, ili kuepusha hasara kwa wafanyabiashara ambao walikuwa tayari wamefanya mipango yao kabla ya mabadiliko ya kodi kutangazwa.
 
Back
Top Bottom