Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Mkuu Britannica, asante kwa taarifa hii, kwenye ukweli unaleta za kweli kabisa tena za Moto moto kutoka jikoni, ila pia ni mpishi mzuri, ukiamua kupika, na viungo unavyo pikia, pilau na biriani zitasubiri, kama ile ya kisiwa cha Guam.
P
Unataka useme nn mkuu?
 
Mkuu nadhani umekariri tu,kuna mabadiliko sana kwa sasa! Mimi ni muathirika wa hii issue. Niliuza nyumba yangu mkoani zaidi ya 60mil. Me nilikuwa na akaunti yangu kwenye bank ambayo haina branch huko. Nikalazimika kufungua akaunti kwenye moja ya hizi bank zenye nasaba na serikali. Na wakati nafungua nilijieleza km nalipwa pesa za kuuza nyumba yangu. Na mtu aliyekuwa ananilipa ana akaunti hapohapo ktk ile bank. Nilifanya taratibu zote na pesa ikaingizwa. Baada ya siku 2 nilifanikiwa ku-withdraw milioni 3 na nusu. Na nikarudi dar. Nimefika dar nimekaa km wiki moja,nikaenda kumlipa mtu milioni 35 za nyumba ambayo nilitaka kununua hapa mjini. Nikakuta nimepigwa pin. Yaani mpaka hv nnavyoandika nimeshapeleka vielelezo vyote nilivyoombwa lkn bado sijaruhusiwa kutumia pesa zangu mwenyewe. Na ni kesi ya tangu mwaka Jana mwezi wa 9. Yaani hata kuchukua elf 20 siwezi. Hii nchi imeshaharibika. Nyumba sina na hela sina! Usicheze na jiwe mkuu,ndo maana kila siku anasema hela zipo!
 
Ujamaa huu unaharibu nchii na kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Siujui ni wawekezaji gani watakuja kuwekeza kwenye nchi yenye sera mbovu kama hizi za ujamaa uchwara!
Hakuna kitu cha kijinga kama Communism jamani
 
Zipo Blackmail zinachezwa bank na baadhi ya Polisi na Takukuru wasio waaminifu, hufunga A/C za watu kwa visingizio vya kizushi ili mwenye A/C atoe Rushwa kwa meneja wa Bank, Ujue kila Ubaya ukitengenezwa wapo wajanja hutumia huo mwanya kujinufaisha, Kwa sasa ni mda wa vyombo vya Dola kuneemeka kupitia Ukuda wa mtukufu na Naibu Rais ndugu Bashite, huko mitaani wananchi wa kawaida wanalia njaa lakini wapo wajanja wachache wanapiga pesa kwa kwenda mbele kuliko tawala zote tokea Nchi ipate uhuru, Kufa kufaana.
 

United States of America masharti sio kiasi hiki aisee!

Unbankable population itaongezeka!

Tulisema kitambulisho cha taifa kita-solve everything,ila naona it is useless on every step!
 
Awamu ya tano ni awamu ya kuwatia hofu wananchi kwa miaka yote tokea iimgie madarakani, lakini wajanja wachache wakiwemo mameneja wa mabenk wamepiga pesa za wateja kwa visingizio kuwa A/c zao zinachunguzwa na vyombo vya Dola wamekuwa wakila njama kisha kula pesa za watu, wametumia fursa hizo kujinufaisha na sasa Bank zinazidi kuongeza kero kwa wateja wao unategemea nini zaidi ya wananchi kuendelea kuichukia zaidi Serikali ya mtukufu toka chato?
 
United States of America masharti sio kiasi hiki aisee!

Unbankable population itaongezeka!

Tulisema kitambulisho cha taifa kita-solve everything,ila naona it is useless on every step!
Kama ni kweli kwa spidi hii itafika mahali hata mtu kutoka nyumbani kwako unashindwa maana nako kutawekewa masharti.
 
Kwa kero zao hakuna Mtanzania atazipenda bank tena pia ujue mameneja wa bank wengi wamekuwa wakila njama kufunga A\c za watu kisha kuwachukulia pesa kugawana na wala njama wenzao.
 
Kama ni kweli kwa spidi hii itafika mahali hata mtu kutoka nyumbani kwako unashindwa.

Maana mkuu hakuna maana ya kitambulisho cha taifa sasa!

Maana kile ndio kila kitu,kina SS number,finger prints,your full data on the national database,etc.

Ambapo akiingia anaona kila kitu.Then wanarudi kinyume wanasema Kitambulisho hakina utoshelezi inatakiwa some other things,hivyo hakina maana to begin with!

USA ukiwa na Social Security number to unaaminika kila mahali maana data zako zipo legitimately kwenye system.

Baada ya kurahisisha vitu wanazidi weka vitu vinakua vigumu mnooo!

You know what will happen?

Watu wengi hawataweza kumiliki account,hela nyingi waziweka kwenye mpesa,nk!

Tegemea mobile money volume to triple or quadruple from now on.

Of which it is even harder for government to regulate!

Vikampuni vidogo sana vitahamia mobile money too.Na hivi vikampuni ni vingi!

Mabenki mengi yatakufa,we will see this happen more next year!
 
Mkuu Daudi asante, maana angalau embe lina umbo zuri, dogodogo na liko smooth, ingekuwa umenitukana kichwa kama dafu, nazi au boga, ningekasirika.
P
Pole Paskal hizo ndizo changamoto za mitandaoni, lakini tambua kuwa wananchi wamechoka kunyanyaswa na CCM mpaka wamepagawa sasa
 
Black market itapaa kwa sana.
Crypto currency itapaa pia

Banking inaenda kufa kifo kibaya

Itafata mobile money huko watapiga pin kwenye utoaji wa hela
 
Too bad. Lakini lazima kuna motive behind this, itajulikana au inajulikana tayari. Kuna kitu tu.
 
Twende sawa kwanza, ujamaa si ukomunisti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…