DOKEZO KERO Ongezeko la Viwanda Mkuranga ni mipango ya Serikali au nguvu ya fedha inachukua nafasi yake?

DOKEZO KERO Ongezeko la Viwanda Mkuranga ni mipango ya Serikali au nguvu ya fedha inachukua nafasi yake?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la Viwanda vingi huku kwetu maeneo ya Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.

Taarifa ambazo sio rasmi inadaiwa kuwa mpaka sasa kuna jumla ya viwanda 57 vikiwemo vikubwa sita vya kati 13 na vidogo 38.

Kutokana na uzoefu wangu katika sekta ya Viwanda ninavyofahamu ni kuwa Wilaya ya Mkuranga haijafanya Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira (SEIA) kwenye maeneo yenye viwanda, badala yake wenye viwanda wamekuwa wakinunua ardhi kutoka kwa wenyeji na wakulima na kisha kujenga viwanda.

Hali hiyo inatishia Wilaya kuja kukosa mpangilio wa matumizi ya ardhi yake kwa viwanda, makazi, kilimo, ufugaji na matumizi mengine ya kijamii.

Ninavyofahamu ni kuwa upande wa Viwanda ambapo Serikali ilikuwa ikisisitiza umetengwa kwa ajili ya mpango huo ni Wilaya ya Kibaha.

Sasa hiki kinachoendelea Mkuranga, je ni sehemu ya mpango wa Serikali katika kukuza Uchumi au ni ile kawaida kwamba wenye hela wanakuwa na nguvu ya ushawishi wa kupindisha Sheria au mipango ya Serikali ya muda mrefu?

Upande mwingine ni kuwa vipi kuhusu mazingira ya afya ya kwa Wananchi wa Mkuranga, yapo salama? Wanaotoa ruhusa ya ujenzi wa viwanda wanazingatia hilo?

Pia soma - Ipo siku Mkuranga tutapata msiba wa Taifa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.
 
Back
Top Bottom