Ongezeko la wagonjwa wenye Vimelea vya Helicobacter Pylori nini Shida

"kuambukizwa ni kupitia matumizi ya vitu vyenye vya H-Pylori kama vile maji au vyakula", bila kutumia vitu hivi viwili tusingekuwepo duniani, eleza aina ya vyakula isipokuwa kitimoto iliyochanganywa mchicha na ndizi usihusishe kwani hatutaelewana.
 
Kseli jamani shida kubwa sana tuwe makini masna sasa.....haki mvaya sana....hospitsl kubwa zote wanapata wagonjwa wengi sanaaaa....mfano aga khan kila week wana procedure zaidi 20 ( 2 specialist Dr)....wanafanya endoscopy na colonoscopy.....shida kubwa
 
Hili ni tatizo la dunia ya Tatu wala halina cha umakini wowote.

Watu wajitahidi kutumia anti acid au acid controller ndio watasalimika na kupatwa na hayo madonda ya tumbo.
 

Attachments

  • IMG20240120141007.jpg
    852.4 KB · Views: 25
Hii acid controller inapatikana wapi hapa Tanzania ??....
Mimi nina connection na Marekani naagiza mara Kwa mara.

Hakuna Mmarekani anaweza kukwambia ana vidonda vya tumbo au kaambiwa asile pilau, dagaa au Maharage, huu ni ujinga upo Bongo/Africa.

Kama upo Dar pale Namanga Best bite kuna clinic inaitwa premier care Kwa Dr Pierre check kwenye pharmacy yao huwezi kukosa hizi anti acid tablets, ukitumia hizo huwezi kupatwa na vidonda vya tumbo na aliyepatwa atumie hizo anti acid atakula vyakula vyote na vinywaji vyote.
 
Upimaji wa Hp umeongezeka sana hivyo kuonekana kama vile Hp wameongezeka.
 
Huyo bacteria kitaalamu asili yake ni tumboni,

KAZI ya bacteria huyo ni kudhibiti acid Inayozalishwa tumboni kumeng'enya chakula Ili acid hiyo isiharibu utumbo.

Muhimu ni kubalance acid mwilini Kwa kutumia dawa aliyotaja Dr Matola PhD na pilipili.

Wahindi wanatumia sana pilipili, inasaidia kubalance acid mwilini.

Hata mwenye madonda ya tumbo, tumia pilipili kwenye chakula utanishukuru.
 
Mkuu rabbon kwema, nina vidonda vya tumbo pia hivi karibuni Kuna jamaa kanishauri nitumie pilipili hapa napo naona umetoa ushairi wa pilipili, nakumbuka kipindi cha nyuma wakati pia nilipokuwa na vidonda nilipojaribu mara kadhaa kutumia pilipili nilipatwa na kuendesha sana hilo unalionaje? Na pia pilipili zipo za Aina nyingi kwenye matumizi ni pilipili yoyote au ? Maswali ni mengi naomba nifahamishe hilo Asante
 
Amen asante sana nitapita pale.....inanisumbua sana hii kitu
 
Ikiwa unatumia pilipili na Ina kudhuru, yaweza kuwa madonda uliyonayo yapo stage ya juu zaidi.

Pima ujue stage ya madonda Yako, Mimi niliambiwa kutumia pilipili na mhindi mmoja na sikuamini, nikaanza Polepole kutumia pilipili Ile yenye kupikiwa kwenye mboga yenye harufu nzuri, usitumie pilipili kichaa, na matumizi yawe pole pole.

Muhimu pia, hakikisha huvushi muda wa kula, asubuhi kula Kwa wakati, mchana kula Kwa wakati, na jioni pia.

Usile dagaa, tumia mboga za majani zaidi Hasa mlenda, Samaki nk nk.

Mimi nilikuwa na madonda ambapo nilikuwa nikivusha tu muda wa kula, napata shida sana.

Mimi ni mtumishi wa Mungu pia, Kwa kuwa nilikuwa na madonda, sikuweza KUFUNGA, niliepuka KUFUNGA.

Tangu nilipojiweka karibu zaidi na Mungu, na kupewa moyo wa kuachilia, kusamehe na kutoweka visasi moyoni, stress ziiniondoka ambazo ni chanzo kikuu Cha magonjwa ya tumbo.

Now naweza KUFUNGA bila shida yoyote, naweza kaa masaa zaidi ya 12 bila kula, hata Leo Jumamosi nimefunga na sipati shida yoyote,

Naweza kula maharage, dagaa, maziwa nk nk

Ninakuombea Mungu akuponye kama alivyonisaidia Mimi.

Ubarikiwe.
 
Uandaaji wa vyakula migahawani haukidhi viwango vya uandaaji wa chakula. Watu wengi wamejiajiri kwenye hilo eneo lkn hawakidhi vigezo vya usafi. Watu wengi tumekuwa tukila migahawani kutokana na kukosa muda. Muda mwingi unachukuliwa na kufukuzana na shekeli.
Chukulia kwa mfano kachumbari ambayo huandaliwa na kutumika bila kupitia kwenye joto lolote. Maanake kama H-Pylori walikuwepo kwenye maji ya kuoshea au mikono ya muandaaji, watamezwa wakiwa wazima kabisa kwenye kachumbari.
Maji ya kunywa na maji ya kunawa mahali pengine haifuati kanuni za afya.
 
Anhaaa, sasa napata connection. Kuna dogo mmoja kule Buzuruga, Mwanza aliniambia kuwa yeye alikua anasumbuliwa na vidonda vya tumbo akawa akila pilipili anaumia sana lakini baadae anakuwa poa. Akawa anazila kwa fujo tumbo likiuma kisha linatulia.
Baadae akanipa habari ile hali ya tumbo kujaa gesi, kuunguruma, kuharisha imeisha. Anakula maharage, dagaa na kila kitu. Kiufupi alipona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…