Ongezeni mabasi ya kutoa huduma ya usafiri DART Stendi Kuu ya Kimara Mwisho, watu ni wengi na mabasi ni machache

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Kero ya usafiri Kimara Termina ni kubwa sana muda wa kuanzia asubuhi mpaka saa 6 mchana.

Msongamano wa watu ni mkubwa sana na mabasi yenu ni machache.

Toeni tenda watu binafsi waingize mabasi kwenye hii njia yenu, maana inaonekana kazi imewashinda.

Leo tena inajirudia karaha ya siku zote, abiria wanasota vituoni korogwe na Kimara kwa zaidi ya masaa mawili wakisubiri gari yenye nafasi wapande waingie katika uzalishaji mali na kuliendeleza taifa.

Binafsi nimefika kituoni saa moja asubuhi mpaka saiz saa tatu na nusu sijaweza kupanda kwenye gari. Hii sio mara ya kwanza. Ni Bora kama wenye dhamana ya kutatua kero hii wakae pembeni wanatukwamisha katika maendeleo kama taifa.

Wanafunzi wanafika shuleni saa 4 kisa usafiri tabu, wananchi wanashindwa kuwahi kazini. Hivi ni kweli kabisa hili haliwezekani kutaftiwa ufumbuzi?

Kama LATRA walisema hao jamaa hawawezi kuwawajibisha basi hakuna kitu hapo.CAG aliwahi toa taarifa kuhusu Mwendokasi watu wameiweka mfukoni usitegemee kitu kipya tena..
 
Kero kubwa sana watu wanakaa kwenye foleni zaidi ya saa nzima.Cha ajabu mabasi mengine yanafika na kuegeshwa pembeni bila ya kuchukua abiria
 
Wamekusikia Mkuu, wasipokusikia ni wajeuri.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Leo tena inajirudia karaha ya siku zote, abiria wanasota vituoni korogwe na Kimara kwa zaidi ya masaa mawili wakisubiri gari yenye nafasi wapande waingie katika uzalishaji mali na kuliendeleza taifa.

Binafsi nimefika kituoni saa moja asubuhi mpaka saiz saa tatu na nusu sijaweza kupanda kwenye gari. Hii sio mara ya kwanza. Ni Bora kama wenye dhamana ya kutatua kero hii wakae pembeni wanatukwamisha katika maendeleo kama taifa.

Wanafunzi wanafika shuleni saa 4 kisa usafiri tabu, wananchi wanashindwa kuwahi kazini. Hivi ni kweli kabisa hili haliwezekani kutaftiwa ufumbuzi?

Balaa sana mzee baba
 
Wewe ukiteukiwa unaweza kutatua?
Pesa wanazozikusanya kwa siku ni nyingi mno...basi moja linabeba zaidi ya watu 100...nauli ni 750 hawana mshindani katika njia zao wala hakuna foleni kusema gari zitakula sana mafuta
 
Kero ya usafiri Kimara Termina ni kubwa sana muda wa kuanzia asubuhi mpaka saa 6 mchana.

Msongamano wa watu ni mkubwa sana na mabasi yenu ni machache.

Toeni tenda watu binafsi waingize mabasi kwenye hii njia yenu, maana inaonekana kazi imewashinda.
Ninacho shauri Mwendokasi wameshindwa kukidhi mahitaji ya kusafirisha abiria, naomba LATRA waruhusu mabasi ya DALADALA rout ya MBEZI POSTA/ KIMARA POSTA KIMARA KIVUKONI na MBEZI KARIAKOO zote ziwe Via MOROGORO ROAD.ingebust shida ya abiria wa mwendo kasi, sababu kwakweli Wamechemka sNaa
 
Back
Top Bottom