Kila kitu akatika maisha ni kamari
1. Unakuwa na malengo ya kilimo una invest pesa nyingi lakini hali ya hewa inakataa pesa yote imeisha ( mkeka umechanika)
2. Unakuwa na wazo la biashara una invest fedha nyingi za matengenezo na miundo mbinu ya hiyo biashara mwisho wa siku wateja hakuna (mkeka umechanika)
3. Unahamasika kusoma ili uje upate kazi nzuri, unakesha usiku kucha wazazi wanauza kila kitu mwisho wa siku matokea zero (mkeka umechanika)
4. Unakuwa na hamasa ya kuwa na mke mwema , tena unashauriwa nenda kijijini kwako ukaoe kabila na mshika dini yako...kweli unampata siku za mwanzo mnaheshimiana lakini baadaye unasikia washkaji wanajimegea bila aibu ....(mkeka umechanika)