Chadema issue siyo wafuasi na wapiga kura. Tatizo ni kwamba hata chadema ikishinda ccm wanapora ushindi.
Kwahiyo mapambano yaelekezwe kwenye upatikananji wa katiba mpya na hatimaye tume huru ya uchaguzi.
Mkuu 'Sex', tunarudiarudia haya haya kiasi kwamba hadi yanapoteza maana halisi.
Ninakubaliana na wewe moja kwa moja, kwamba kwa hali ya sasa, CHADEMA tatizo si kuishinda CCM, kwa sababu hili lipo wazi kabisa kwa wakati huu.
"CCM kupora ushindi" - hili ndilo tunalowahimiza CHADEMA walifanyie kazi usiku na mchana kwa sasa; kukomesha kabisa tabia hiyo ya CCM.
"CCM kupora ushindi" siyo swala la Katiba linaloruhusu uporaji wa kura. Hata hii Katiba mbovu tuliyo nayo sasa hivi, haiwaruhusu CCM kupora kura; na nijuavyo mimi, hakuna sheria yoyote inayowapa ruhusa CCM kupora kura.
Kwa hiyo, tabia hiyo ya CCM ni UHARIFU. CCM wanavunja sheria na Katiba iliyopo sasa wanapopora kura.
Sasa swali la kujiuliza, inakuwaje watu tukafikia hatua ya kudhani kuwa CCM kupora kura ni halali yao kufanya hivyo?
Kwa nini nchi nzima imechukulia jambo hili la kiharifu liwe kama jambo la kawaida linapofanywa na CCM?
Ninachopendekeza mimi, ni kwa CHADEMA kulifanyia kazi jambo hili, na hasa hasa kulifikisha kwa wananchi walielewe vyema, na wananchi hao wawe sehemu ya kukataa UHARIFU unaofanywa na CCM.
Hii ndiyo kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya CHADEMA wakati huu na kuendelea hadi kufikia chaguzi za 2024/2025.
Huku kulilia Katiba Mpya, pamoja na kuwa jambo jema, lakini hakuna manufaa yoyote kwa muda huu uliopo sasa. CCM wenyewe wamekwishajihakikishia kuwa hili siyo swala tena kabla ya chaguzi hizo zinazofuata.