Oparesheni 255: Tundu Lissu afanya mikutano 5 Bariadi Vijijini

Oparesheni 255: Tundu Lissu afanya mikutano 5 Bariadi Vijijini

Huyu Lisu,ni binadamu mwenye IQ ya kipekee kabisa,na Mkono wa Mungu upo juu yake,kuna kazi maalumu alipewa na Mungu kulisemea taifa bila woga wowote.Binafsi 2025 asimame na ipeperushe bendera kwenye mbio za uraisi tena.2020 japo kwenye karatasi ya kupigiwa kura aliwekwa mwishoni yaani sikuchukua sekunde kutia tick kwenye jina Lake,nikaindumbukiza kwenye kisanduku ,sikujali kura yangu either itapotea au kufanywa tofauti na wenye nguvu,nilipiga kura kwa mguso wa ndani kabisa dhidi ya viongozi dhalimu waliokuwepo kipindi hicho.Heko Lisu, mpigania maslahi ya wengi.
 
Kila jambo na wakati wake.
Mwakani kuna uchaguzi wa serikali za mitaani na mwaka unaofuata uchaguzi mkuu. Kwahiyo muda wa kusubiri hakuna na muda kuipata katiba ni sasa
 
"CCM kupora ushindi" siyo swala la Katiba linaloruhusu uporaji wa kura. Hata hii Katiba mbovu tuliyo nayo sasa hivi, haiwaruhusu CCM kupora kura; na nijuavyo mimi, hakuna sheria yoyote inayowapa ruhusa CCM kupora kura.
Ni kweli katiba hii mbovu haiwaruhisu ccm kupora kura na uchaguzi, lkn haiwabani . Haiwabani kwasabb rais na mwenyekiti wa ccm yuko juu ya katiba, anaweza kufanya lolote ikiwemo kupora kura na hawezi kushtakiwa wala kuhojiwa na chombo chochote hapa nchini.
 
JamiiForums753274111.jpeg
 
Mkuu 'Sex', naelewa unachokizungumzia hapa, wala usiwe na shaka juu ya hili.

Ninachosema mimi, huyo huyo Rais hana mamlaka yoyote juu ya wananchi.
Anaweza kukiuka hiyo katiba mbovu, siyo kuwa sheria inamruhusu, bali kwa ukaidi tu; lakini rais huyo huyo kaidi hana uwezo wa kukaidi uamzi unaofanywa na wananchi.
Nami ninakuomba unielewe juu ya hili, kama mimi ninavyokuelewa vizuri sana juu ya Rais kaidi wa sheria na Katiba.
 
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema , Tundu Lissu leo amevurumisha mikutano 5 mfululizo kwenye jimbo moja tu la Bariadi Vijijini

Kama Kawaida yake , Lissu amewaomba Wananchi waunge mkono chama chake ili Katiba mpya ipatikane sasa badala ya porojo za viongozi wa serikali akiwemo Damas Ndumbaro

Amesema Katiba Mpya itazuia wananchi kuporwa migodi yao .

Hii hapa ni kata ya Nkololo.

View attachment 2735847View attachment 2735848
Huyu jamaa ana energy
 
Mkuu 'Sex', tunarudiarudia haya haya kiasi kwamba hadi yanapoteza maana halisi.
Ninakubaliana na wewe moja kwa moja, kwamba kwa hali ya sasa, CHADEMA tatizo si kuishinda CCM, kwa sababu hili lipo wazi kabisa kwa wakati huu.
"CCM kupora ushindi" - hili ndilo tunalowahimiza CHADEMA walifanyie kazi usiku na mchana kwa sasa; kukomesha kabisa tabia hiyo ya CCM.

"CCM kupora ushindi" siyo swala la Katiba linaloruhusu uporaji wa kura. Hata hii Katiba mbovu tuliyo nayo sasa hivi, haiwaruhusu CCM kupora kura; na nijuavyo mimi, hakuna sheria yoyote inayowapa ruhusa CCM kupora kura.

Kwa hiyo, tabia hiyo ya CCM ni UHARIFU. CCM wanavunja sheria na Katiba iliyopo sasa wanapopora kura.
Sasa swali la kujiuliza, inakuwaje watu tukafikia hatua ya kudhani kuwa CCM kupora kura ni halali yao kufanya hivyo?
Kwa nini nchi nzima imechukulia jambo hili la kiharifu liwe kama jambo la kawaida linapofanywa na CCM?

Ninachopendekeza mimi, ni kwa CHADEMA kulifanyia kazi jambo hili, na hasa hasa kulifikisha kwa wananchi walielewe vyema, na wananchi hao wawe sehemu ya kukataa UHARIFU unaofanywa na CCM.
Hii ndiyo kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya CHADEMA wakati huu na kuendelea hadi kufikia chaguzi za 2024/2025.

Huku kulilia Katiba Mpya, pamoja na kuwa jambo jema, lakini hakuna manufaa yoyote kwa muda huu uliopo sasa. CCM wenyewe wamekwishajihakikishia kuwa hili siyo swala tena kabla ya chaguzi hizo zinazofuata.
Daah saitakuwaje
 
Daah saitakuwaje
Jibu ni kuwaelimisha na kuwategemea wananchi wenyewe kuamua.

Kazi iliyopo ni kuwapa elimu wananchi wasikubali haramu ya CCM kuiba kura, au kutumia mabavvu kubaki madarakani.
Wananchi wakikataa hilo, hakuna mwenye nguvu ya kuwazuia.

Nionavyo mimi, wananchi wapo tayari kabisa kuifanya kazi hiyo.
 
Watanzania wanamwelewa sana Mh. Lissu, na ki ukweli ndiye Rais wao kama si uchakachuaji wa uchaguzi na kupindua matokeo.
 
Kuwa wa kwanza kufahamu kwamba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema , Tundu Lissu leo amevurumisha mikutano 5 mfululizo kwenye jimbo moja tu la Bariadi Vijijini

Kama Kawaida yake , Lissu amewaomba Wananchi waunge mkono chama chake ili Katiba mpya ipatikane sasa badala ya porojo za viongozi wa serikali akiwemo Damas Ndumbaro

Amesema Katiba Mpya itazuia wananchi kuporwa migodi yao .

Hii hapa ni kata ya Nkololo.

View attachment 2735847View attachment 2735848
Shida ya Matanzania ni kukosa Shule,
Hapo yamekusanyana ka yanaelewa hoja vile, CCM wakipita wanakokotwa tena ka Ng'ombe.
Uchaguzi ingekua kesho ningejipa Moyo ila mpaka 2025 yatasahau tu.
Tuombe Wasigawiwe tu Vitenge na Kofia za Kijani na Njano.
Usaliti wa JMTz unaanzia ngazi ya Cell>Individual>Familia>Chama>Taifa.
 
lakini rais huyo huyo kaidi hana uwezo wa kukaidi uamzi unaofanywa na wananchi.
Ktk hili nakuelewa lkn wananchi walio wengi Wana dhana kwamba kura zikiibiwa ni hasara ama pigo kwa mgombea na siyo wananchi wenyewe
 
Shida ya Matanzania ni kukosa Shule,
Hapo yamekusanyana ka yanaelewa hoja vile, CCM wakipita wanakokotwa tena ka Ng'ombe.
Uchaguzi ingekua kesho ningejipa Moyo ila mpaka 2025 yatasahau tu.
Tuombe Wasigawiwe tu Vitenge na Kofia za Kijani na Njano.
Usaliti wa JMTz unaanzia ngazi ya Cell>Individual>Familia>Chama>Taifa.
Msimu huu hayo hayatafanikiwa
 
Ktk hili nakuelewa lkn wananchi walio wengi Wana dhana kwamba kura zikiibiwa ni hasara ama pigo kwa mgombea na siyo wananchi wenyewe
Hapo sasa ndipo wanapotakiwa CHADEMA kukazia elimu kwa hawa wananchi na kutumia mifano rahisi kabisa ambayo sasa ipo mingi na ni rahisi kueleweka kwa wananchi wote.

Mfano: ni mwananchi gani asiyejua hujuma iliyoshiriki Bunge na wabunge wote kutaka kupitisha haramu ya DP World?
Ni mtu gani asiyeweza kuelewa hili?
Mifano mingi sana ya namna hii ipo inayoweza kutumiwa na CHADEMA kuwafundisha wananchi.
 
Back
Top Bottom