Opinion: Dr. Shika Ana Hali Fulani, Anahitaji Msaada, Huruma, Upendo na Protection of His Right to Privacy!.

Exactly...[emoji106]
 
Nikweli jamaa dishi limecheza, lakini ana mengi yaliyojificha kiasi cha kuhitaji msaada sio kutoka kwa jamii bali vyombo vya usalama, waliomvuruga akili wakimuona namna anavyojieleza na kuficha baadhi ya vitu ambavyo kwa mtu ambaye dishi limecheza asingeweza kuficha wanaweza kumuwinda tena na kuhatarisha usalama wake.

Vyombo vya usalama pekee ndivyo vyenye uwezo wa kumlinda huyu jamaa na kulifunga hili suala kwenye vyombo vya habari maana inaweza isiwe salama kwa dr, Binafsi naona kabisa huyu jamaa ni dumped agent wa CIA ambaye ni liability kwa CIA lakini ni asset kwa kGB...
 
I concur with u Pascal, time will tell
 
Ni kweli anaweza kuwa ni insane or the opposite,mimi nimeshawahi kuwa na mtu wa karibu yangu,wanaomjua wanasimulia kuwa alikuwa genius kipindi cha ujana wake,lakini navyosikia baadaye akaja kupata hilo tatizo la akili.Ni mtu aliekuwa akitoa usaidizi mpaka kwa baadhi ya wanasheria akiwa katika hiyo insainity na walikuwa wakimlipa kwani profession yake alikuwa ni lawyer.Ni kitu kimoja tu kilikuwa kinamfanya uweze kugundua kuwa ana tatizo la akili,alikuwa haogi mpaka aambiwe na nguo pia habadilishi bila ya kumwambia,lakini anaondoka asubuhi kama anaekwenda kazini,lakini hajulikani anakokwenda,na akirudi anakuwa na gazeti la siku ile,na ana habari zote za siasa au za kiuchumi za siku husika na anazisimulia kwa ufasaha kabisa.Kwahiyo yawezekana hata Shika akawa hayuko vizuri,lakini kama hajapimwa ni nani anaeweza kusema kuwa hana akili kwa kumuangalia tu...
 
Huyu dk inahitaj tumpe nafas nyingine ya kumsikiliza before kujua kwamba ni insane or not, ukiangalia trend ya mahojiano siku nyumba inauzwa na hii ya wiki hii maswali yanazid kujaa kichwan, anajib maswal kiufasaha na kwa utuliv mzur tu though sometimes story zake hazina connection... Lakin nakueleza pascal huyu mtu sio wa kumuundermine.
 
Mi sina jipya zaid ya kusisitiza jamaa alikuwa agent wa CIA Kuhusu akili yake inasemekana alikuwa injected some materials ya kuwewesesha akili yake, na anaonekana yeye kuficha mambo mengi mno
 
Wakati wa zama za Cold War na Tanzania chama kilishika hatamu. U communist ulienezwa katika developing world na vijana walipata nafasi kwenda kusoma elimu ya juu katika nchi za ki-communist kama Cuba, China, Russia na kwingineko.

Katika waliokwenda Russia kuna wakioombwa kujiunga na KGB na walipewa mafunzo na posho kidogo. Wengi wakijua ni kwa kipindi wako Urusi tu wakimaliza shule wanaachana nao.

Kuna familia si wezi kuitaja kwa jina, kaka yao mkubwa alirudi mzima kumbe aliwakimbia KGB bila kufahamu ukijiunga ni kwa maisha yako yote.

Yule kaka aliuliwa kwa risasi Bahari Beach Hotel alipokuwa anakaa akisubiri nyumbavya serikali. Mpaka kesho hajulikani aliyemuua. Rumours has it KGB walimaliza.

Waliokuwepo Dar miaka ya 80 watakumbuka hili tukio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…