Opinion: Dr. Shika Ana Hali Fulani, Anahitaji Msaada, Huruma, Upendo na Protection of His Right to Privacy!.


paskali ameandika vizuri tu. Je unataka utafuniwe? read between the lines
 
Nimefuatilia mahojiano yake. Nimebaini ana hazina nzuri tu itakayoweza mtoa hapa alipo. Angepata ma editors wa movie wa kimataifa mfano Hollywood angewapa story yake wakaitengenezea movie kali ya kijasusi naimani ingemlipa sana. Na ingekua ni movie nzuri mno kuwahi kutokea. Bahati mbaya kaangukia kwa erik shigongo naimani tujiandae kusoma hadithi nzuri za kijasusi.
 
Dr Louis Shika ni mtu makini anayejielewa sana ila kwa wale waliokuwa wanakimbilia kujibu maswali ya kuchagua shuleni watamuona kama kichaa.. ni mtu mwenye utimamu wa kipekee angalia anavyojibu Maswali kwa umakini kabisa...
 
Mambo ya msingi tumekatazwa kuyajadili au hukusikia marufuku toka kwa bosi wa sumatra?
 
Bila kupepesa macho nitaungana na maelezo yake kuwa nalitekwa na majambazi waliokuwa wakitaka awape fedha kiasi cha $1.5 mil......

Kuthibitisha hili ndio maana alitamka baada ya kupata msaada alipelekwa police na polisi hao hao kumsaidia kuwatafuta wale majambazi.

To my sense, ingekuwa kile kikundi kingekuwa ni KGB basi asingepata msaada wa police Otherwise awe amepindisha yeye mwenyewe maelezo ya jinsi tukio zima lilivyotokea.

MY TAKE: Pamoja na haya mawazo yangu. Bado nasisitiza haya ni mawazo ya awali sana. Kuna vitu vingi sana vimejificha havijajibiwa maswali yake hivyo maoni haya yanaweza yasiwe hivyo kama nitapata fursa ya kujua vitu vingi ambavyo bado najiuliza.

Kifupi tu niseme, taarifa kutoka kwa aliyekuwa balozi wa tz nchini Urusi kipindi hicho bado bado imeendelea kunifanya niwe na maoni haya!
 
Tangua arejee kutoka Urusi hajawahi kwenda kijijini kwao
Kumbuka wazazi wake walifariki akiwa urusi na walimsomesha kwa shida sana
Ndugu zake hawakujua yuko wapi hadi hii issue ya juzi
So nahisi hayuko vizuri upstairs
 
Mayala
Pata nafasi umu interview Dr shika nahisi ana mambo mengi na makubwa sana
Historical background yake na vituko alivyopitia naamini makala za ajabu zaidi y a mia zitapatikana
 

Ulimsikia akiwataja KGB? Unaikumbuka KGB?
 
Nimefuatilia sana maelezo ya huyu bwana kwa makini sana.Nilianza siku ya mnada wa Nyumba za Lugumi,maelezo aliyotoa polisi kuhusu mnada, Jinsi alivyotambulisha kampuni yake na alivyotekwa Urusi.

Kutokana na maelezo ya watu mbalimbali katika mijadala mbalimbali wakidai jamaa ni chizi kwangu hazina mantiki.Iweje chizi awe na kumbukumbu kiasi hiki!!!!!

USHAURI:
Shika ni mtanzania mwenzetu sasa kuna haja serikali ikafuatilia diteili zake na kuweza kumsaidia.Kwa kufanya hivyo tutaweza kujua Urusi kwa nini walimtesa na kumkata vidole hii inauma sana.
 
Dr Louis Shika ni mtu makini anayejielewa sana ila kwa wale waliokuwa wanakimbilia kujibu maswali ya kuchagua shuleni watamuona kama kichaa.. ni mtu mwenye utimamu wa kipekee angalia anavyojibu Maswali kwa umakini kabisa...
Kuna maswali mengi sana ambayo hayajajibiwa, kwanini?
 
Naunga mkono hoja, sio tuu media zimempa undue attention, bali sijasikia hata madia moja ikimhoji very serious things, anazungumzia viti vya kufikirika tuu kwa kutunga, watu wanamwamini, anasema alitoroshwa Urusi kwa msaada wa watu wa Marekani, ukweli Balozi Chokala kautoa, alipata insanity akiwa Urusi, akajitapa ana pesa, akatekwa, akateswa, serikali ikamrudisha kwa siri chini ya ulinzi mkali, akakabidhiwa nchini.
  1. Amedanya kumiliki kampuni na fedha nyingi, media zimedanganyika badala ya kuhoji how, amewezaji kumiki hiyo kampuni kwa capital gani?!.
  2. Amedanganya kuhamia Holland for 8 years, hawakumuuliza amewezaje with what means?!.
  3. Amedanya ameitwa UNHCR kuwa commissioner akatata, how?!.
  4. Media zimenfuatilia akilipa bima ya bank ili ku transfer funds, tangu lini bank zikalipwa kwa paypal or western union badala ya TT transfer, mtu sio mzima, kakutana na matapeli wa online wanamwingiza mjini, na media zinamsindikiza kuingizwa mjini!.
  5. Mtu ana degree nne hadi Ph.D, wanamcheza michezo ya kuigiza na kupiga pesa kupitia umaarufu wake wakati wanajua fika he is not a comedian, ni mgonjwa!.
  6. Wapiga deal wanampandisha ndege, anapokelewa na gari la wazi, anapungia upepo huku media wanamrekodi na kuja kuonyesha, huku ni kumdhalilisha!.
  7. Kama kwa macho tuu unamuona ni mgonjwa, lakini watu wanamfanya mgeni rasmi!, amini usiamini, kwa Watanzania tulivyo na ignorance tuliyonayo, akigombea, anaweza kupata kura na watu mkashangaa!.
Paskali
 
Atleast umeniconvice kwa comment yako mkuu kama vp jipongeze na chibuku mbili ntalipa kwa cheque
 
Sikuungi mkono hata kidogo. You look biased probably due to etthnicity! Type ya kina Shika (Dr.?) wako wengi sana nchi hii. Ingekuwa mtu mwingine
Mi nafikiri hata huu uzi una kiwango fulani cha insanity, tunapaswa kumuonea huruma mtoa mada pia
You are right. On top Pascal anaonekana kuwa biased,nafikiri ni grounds za ethnicity! Angekuwa wale kabila fulani ninavyohisi,kusingekuwa na attention zaidi ya kuitwa tapeli na kesi nyingi angefunguliwa. Kwa nini nasema hivyo,kina Shika (Dr.?) wapo wengi hasa waliojikuta life status haiendani na matatajio waliyojiwekea. Pili,maelezo ni mengi bila uthibitisho only kwamba kwa hisia zangu,anatoka kulee anakotoka mwenye magorofa na wengineo wenye mwelekeo mmoja. 3. If at all,investigation was genuine,tungeanza na majirani na ndugu zake,mawasiliano yake nk hasa kipindi kabla hajajitokeza katika mnada ule wa maghorofa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…