Oreshnik: Silaha mpya tishio iliyotumiwa na Urusi. Hakuna mfumo unaweza kuzuia duniani, isipokuwa S550 wa Urusi wenyewe

Oreshnik: Silaha mpya tishio iliyotumiwa na Urusi. Hakuna mfumo unaweza kuzuia duniani, isipokuwa S550 wa Urusi wenyewe

Marekani yapewa taarifa na Russia dakika 30 kabla, Ukraine na washirika wake washindwa kuizuia.

Ina uwezo wa kufika na kuangamiza mahali popote Ulaya nzima.

Hakuna mfumo wa kuizuia.

Ni Hypersonic hivyo inaweza kusafiri kwa kasi ya Mach 10 (kilometa 3 kwa sekunde, huwezi kuiona muenendo wake wa kasi kwa macho).

Inabeba vichwa vingi kwa mara moja ambavyo vikitawanyika huko angani kila kimoja kinaweza kujiongoza kufuata 'target' yake sehemu tofauti na vichwa vingine.

Russia imesema itakuwa inatoa taarifa kabla haijafanya shambulizi, tahadhari kwa raia eneo inalotaka kulishambulia waweze kuondoka lengo likiwa kupunguza maafa kwa raia wasiokuwa na hatia.

Muelekeo wa vita kati ya Ukraine na Russia umechukua sura mpya baada washirika wa Ukraine kuruhusu silaha za masafa marefu walizo wapa Ukraine zitumike kushambulia ndani ya ardhi ya Russia inayotambuliwa kimataifa.

Baada ya Ukraine kuzitumia hivi karibuni Russia amejibu mapigo kwa kuifanyia majaribio silaha yake mpya Oreshnik.

Ni teknolojia mpya ya Hypersonic Intermediate range ballistic missile.

Ina uwezo wa kubeba vichwa vya nyukilia (nuclear payload), kwa sasa imetumia vilipuzi vya kawaida(conventional bomb) lengo kutoa onyo tu. Pentagon wakiri silaha hiyo ni tishio lakini wana amini Ukraine itaweza kuhimili maafa yake.

Naomba wale wadau wa mambo ya silaha waje watoe maoni yao. Narudia, wale wadau wanaojua mambo ya silaha siyo shabiki wa vita vya Ukraine au NATO na Russia.

CC: T14 Armata waite wadau wengine tujadili wengine tujifunze.
Kwahiyo wewe siraha zote Dunian unazijua we popoma??
 
Hapo hamna kitu kipya hizo teknolojia zipo tangu miaka ya 1980s.

Multiple Independent Reentry Vehicles (MIRVs) zipo kwa makombora mengind ya Urusi, Marekani na nchi chache. Nchi ya kwanza kutengeneza MIRVs ni Marekani ambayo kutokana na mkataba wa silaha za nyuklia START II Marekani ilipanga kuachana na MIRVs 2014, ingawa haizuii kuendelea. Hata Urusi kuna muda waliacha na sasa ndio wakitaka waendelee.

Kuhusu silaha kuzuilika. Urusi yenyewe ina makombora ya tangu 1970s ambayo ukiwaambia wayafyatue kisha wayadungue kwa mifumo yao ya 2020s hawawezi. Missile tech inaenda kwa kasi zaidi kuliko anti-missile tech. Kutengeneza sumu ni rahisi sana kuliko kutengeneza dawa ya sumu. Urusi haina mfumo wa kuzuia ICBM hata liwe la Pakistan.
Bwashee tatizo sio MIRVs ila Shido ni speed and accuracy ku hit target,kwasasa technology ya silaha za kivita zinawekeza zaidi kwenye utafiti kuhusu speed
 
Marekani yapewa taarifa na Russia dakika 30 kabla, Ukraine na washirika wake washindwa kuizuia.

Ina uwezo wa kufika na kuangamiza mahali popote Ulaya nzima.

Hakuna mfumo wa kuizuia.

Ni Hypersonic hivyo inaweza kusafiri kwa kasi ya Mach 10 (kilometa 3 kwa sekunde, huwezi kuiona muenendo wake wa kasi kwa macho).

Inabeba vichwa vingi kwa mara moja ambavyo vikitawanyika huko angani kila kimoja kinaweza kujiongoza kufuata 'target' yake sehemu tofauti na vichwa vingine.

Russia imesema itakuwa inatoa taarifa kabla haijafanya shambulizi, tahadhari kwa raia eneo inalotaka kulishambulia waweze kuondoka lengo likiwa kupunguza maafa kwa raia wasiokuwa na hatia.

Muelekeo wa vita kati ya Ukraine na Russia umechukua sura mpya baada washirika wa Ukraine kuruhusu silaha za masafa marefu walizo wapa Ukraine zitumike kushambulia ndani ya ardhi ya Russia inayotambuliwa kimataifa.

Baada ya Ukraine kuzitumia hivi karibuni Russia amejibu mapigo kwa kuifanyia majaribio silaha yake mpya Oreshnik.

Ni teknolojia mpya ya Hypersonic Intermediate range ballistic missile.

Ina uwezo wa kubeba vichwa vya nyukilia (nuclear payload), kwa sasa imetumia vilipuzi vya kawaida(conventional bomb) lengo kutoa onyo tu. Pentagon wakiri silaha hiyo ni tishio lakini wana amini Ukraine itaweza kuhimili maafa yake.

Naomba wale wadau wa mambo ya silaha waje watoe maoni yao. Narudia, wale wadau wanaojua mambo ya silaha siyo shabiki wa vita vya Ukraine au NATO na Russia.

CC: T14 Armata waite wadau wengine tujadili wengine tujifunze.
Hakuna Rang wataacha kuona SOMA HAPA
 
Putin ni mtu mwenye busara sana. Anaonekana pia kuwa ni mpole. Angekuwa kichaa fulani hivi na ameshapata sababu ya kutumia nyuklia, angetest.

Ila naona anaamua kuvutavuta mpaka January Trump ayamalize.. vita ya nulcear haina mshindi wote sisi tutafukiwa ardhini sasa ya nini?
 
Hii niliisema zamani kwenye FB na sio bye bye tu na itavunjika vipande vipande zile state 54 zitataka kila moja iwe nchi kamili na serikali zake usa itakuwa nyumba ya buibui 9Bayti ankabut)
Marekani ipo saana
 
Amerika isiondoke hatuwez kuzamia russia au china ,tuendelee kuiombea amerika kimbilio la maninja wazamiaji
America haiwezi kuondoka, itakuwepo karne nyingi zijazo.
Nguvu zake za ushawishi na mabavu dhidi ya mataifa mengine ndiyo vitaondoka au kupungua kwa kiasi kikubwa miongo michache ijayo.
 
Putin ni mtu mwenye busara sana. Anaonekana pia kuwa ni mpole. Angekuwa kichaa fulani hivi na ameshapata sababu ya kutumia nyuklia, angetest.

Ila naona anaamua kuvutavuta mpaka January Trump ayamalize.. vita ya nulcear haina mshindi wote sisi tutafukiwa ardhini sasa ya nini?
Tatizo watu waliochoka kuishi ambao wanataka kufa wamechanganyikana na watu wastaarabu ambao wanapenda kuendelea kuishi ndio maana Putin anakausha.Mfano ni kule Kursk kama wangebaki tu watu wanaotaka kufa ambao wamechoka kuishi tungesawazisha mji wote na baadae tukajenga upya kama Mariupol
 
Silaha zote hufanyiwa majaribio aidha kwa watu wake (wanajeshi) ama nchi nyingine
Mpaka hydrogen bomb wamefanyia majaribio sehemu nyingi hawa wote wenye hizi silaha
Siku hizi ukisikia matetemeko ya Ardhi basi mengi yanafanywa na hawa underground
Hapa Putin amesema atakashusha haka kakisiwa ka 🇬🇧 kwa makombora makubwa sasa sijui ndio haya mabomu anataka kutuzamisha nayo?
Mimi ngoja tu nihamie kufuatilia ligi ya ujerumani bundesiliga mana Uk inaenda kuzamishwa so hakutakuwa tena na Man U 😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Mbona Ukraine wamepoa hawajaendelea tena kutumia silaha zao za masafa marefu baada ya jaribio hilo moja tu?
Jana watu waliongea sana as if maeneo ya Ukraine yaliyochukuliwa na Urusi yamerudishwa kwa kushambulia ndani ya Urusi,lkn Leo wote kimya na yule kibaraka analia kwamba Dunia inatazama jinsi Putin amegeuza Ukraine kama uwanja wa majaribio ya silaha mpya.
USA, UK,France, German na wengine wamebaki midomo wazi na wote wamepiga kimya.
 
Hiyo Vita ya Ukraine siyo vya mlengo wa kidini hata chembe moja.
Siyo ya uislam na Ukristo.
Ukraine analishambulia kanisa la Orthodox nchini kwake. Wamarekani na washirika wake wakristo kwanini waunge mkono mtu kama huyo?
Russia ni nchi ya kikristo kiasi kikubwa.
Fuatilia vizuri.
Mimi muandishi wa makala hii siyo muislam. Nimezaliwa familia ya waumini wa ukristo wakatoliki na kubatizwa kanisa katoliki la mitume.
Kanisa Takatifu katoliki la mitume
 
Hata chizi kuna muda akili inakaa sawa kidogo halafu ndio inapotea tena,hivi kama ingekuwa wewe unapigwa missiles kama zile halafu hat mtetezi wako unayemwamini unamuuliza wamenipiga na nini halafu anakwambia hajui ungeacha kuogopa?
Ha ha haa,aisee wewe jamaa ni mtata hatari.
Hali ni Tete kwa kweli,kama baunsa wako anatetemeka inabidi wewe uwe mpole TU.
 
Upo sahihi kuhusu Multiple Independent Reentry Vehicles (MIRVs).
Pia sahihi kuhusu Intermediate-Range Nuclear Forces Treaty (INF Treaty).
Hapo jipya ni uwezo wa teknolojia mpya ya Hypersonic speed ya hizo (MIRV).
Hiyo ndiyo game changer.
Technically kila ICBM ni hypersonic kwenye reentry phase. Kombora likitembea kuanzia Mach 5 linaitwa hypersonic, kila ICBM unayoona ikiingia duniani tena kuelekea kwenye target inakuwa na zaidi ya Mach 5 nyingine zinaenda hadi Mach 20 na hazijawahi itwa hypersonic sababu zinatokea chini zikiwa supersonic.

Hizo MIRVs zenyewe hakuna inayokuja na subsonic au supersonic speed, zote zinakuja hypersonic. Sanasana nchi zinaweza detect ujio wa shambulizi nazo zinatuma mashambulizi. Utaona kila North Korea anapofyatua kombora la mazoezi au majaribio huwa Marekani inajua sababu imeweka powerful radars chonjo kuona kombora likiwa mwanzoni kabisa. Likishaingia anga la nje, uko hakuna friction linakimbia hypersonic speed na linakuja na hiyo momentum duniani. Hapo hakuna Mrusi, Mchina au Mmarekani anazuia.

Pia Urusi haina dedicated anti missile system, hiyo S-500 ni air defense missile ina mambo mengi inaunganisha haiwezi kuwa effective kila kitu. Hapo Kerch ilipowekwa ilinde daraja ilishindwa kuzuia ATACMS missiles wakati hazipo hypersonic.
Dedicated system kama THAAD haizuii ndege, drone wala cruise missiles yenyewe ni kazi nzito za ICBM tu.

Ukiitafuta nchi yenye ICBM zenye uwezo wa kawaida (huwa naamini ni Pakistan) ukaiambia ifyatue makombora alafu ukawaita Urusi na Marekani wazuie kwa wanavyotaka wao. Chances za Marekani kushinda ni kubwa wakiweka Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) na Aegis Combat System kuliko Urusi wakiweka S-500 air defense system.

Hypersonic inakuwa na maana kama kombora linapita anga la duniani mfano cruise missile. Ila kwa ICBM zote huwa ni hypersonic mwishoni
 
Hapo hamna kitu kipya hizo teknolojia zipo tangu miaka ya 1980s.

Multiple Independent Reentry Vehicles (MIRVs) zipo kwa makombora mengind ya Urusi, Marekani na nchi chache. Nchi ya kwanza kutengeneza MIRVs ni Marekani ambayo kutokana na mkataba wa silaha za nyuklia START II Marekani ilipanga kuachana na MIRVs 2014, ingawa haizuii kuendelea. Hata Urusi kuna muda waliacha na sasa ndio wakitaka waendelee.

Kuhusu silaha kuzuilika. Urusi yenyewe ina makombora ya tangu 1970s ambayo ukiwaambia wayafyatue kisha wayadungue kwa mifumo yao ya 2020s hawawezi. Missile tech inaenda kwa kasi zaidi kuliko anti-missile tech. Kutengeneza sumu ni rahisi sana kuliko kutengeneza dawa ya sumu. Urusi haina mfumo wa kuzuia ICBM hata liwe la Pakistan.
Nakubaliana mkuu
 
Back
Top Bottom