Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ze comedy umaarufu umepungua sana, mie nina sababu kadhaa:
1. Kuishiwa na ubunifu
2. Dharau (mfano masanja anaposema kama hupendi ipotezee, wao wanalipwa sisi tunacheka etc)
3. Uongozi usio na VISION na kujua watu wanataka nini
4. Kulewa umaarufu.
Unajua hawa jamaa wametokea uswahilini, sasa wakipita huko wanaona wanakubalika kweli kweli, tatizo la uswahilini ni kuwa hata mdhamini hafaidiki nako sana maana VODACOM watumiaji wakubwa na wenye kuiingizia hela hawapo uswahilini.
Shule jamani shule kitu muhimu sana!!
Ila jamaa ni wajanja, maana Manji yupo atawabeba, lakini atawabeba mpaka lini?
... for my understanding >80% ya dar ni uswahilini....
Wakuu,
Naomba maana ya neno Uswahilini?
Baada ya hapo Mkuu Kimweri tunaomba utupe "source" ya takwimu hizo hapo juu!
yah!!,niKweli inauma sana kuona wanawakejeli hata watu wagonjwa,utafikiri wao wana mkataba na mungu.AGRIIIIIIIIIIIIIII!!!!!!!!!!.sijawahi kufurahia maonyesho ya ze comedy. Sioni kama wanachekesha zaidi ya kunishangaza jinsi wasivyo na ubunifu. Niliwadharau zaidi siku ile walipomkejeli mwanamuziki banza stone ambaye ni mgonjwa kwa kusema amefulia. Yule mwigizaji mfupi akawa anaigiza jinsi anavyokohoa. Yale ni maradhi, huwezi kumtania mtu anayeumwa. Hawana utu hata kidogo!