Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

Najaribu kumpigia Bw.mdogo wangu Seki nimpe ushauri,naye hapokei cmu yangu... Ok lets wait n see...
 
tatizo ninaloliona kwa hawa jamaa ni kwamba walikuja na ubunifu wa hali ya juu sana na watu wakategemea kuwa utazidi kuongezeka,kinyume chake umeaza kupungua na watu wanaiona tofauti hii,kwa sasa ni bahati mbaya tu kwamba hawajatokea wachekeshaji wengine wa kuwazidi tu,vinginevyo tungeshawasahau.walipoaza akina zembwela na vimbwanga vyao tulifurahia na kuona wanafanya vizuri,lakini walipokuja akina wakuvanga tukaona kumbe hawa akina zembwela sio ishu,sasa imefikia wakati hawa jamaa ubunifu ule wa mwanzo umefikia mwisho,kila wakijaribu kuja na mpya haifiki viwango vile vya mwanzoni,achilia mbali kuzidi,
ni kama vile mtoto ambaye anapoaza shule alikuwa anapata alama 90/100, sasa mzazi unategemea aendelee kuongeza lakini haongezi ila ameshuka na sasa yupo kwenye 60/100.
 
Mimi nataka nianzishe kikundi na nikidhamini na nakipeleka pale pale TBC kuwe na vipindi viwili wachuane.

Hawa the comedy hawana mshauri aliyekwenda shule...biashara yoyote lazima shule iwepo la sivyo itakuwa zile biashara za kuhonga TRA na mapolisi (magendo)

Ze comedy hawana shule. Ndo tatizo
 
Ze comedy umaarufu umepungua sana, mie nina sababu kadhaa:

1. Kuishiwa na ubunifu
2. Dharau (mfano masanja anaposema kama hupendi ipotezee, wao wanalipwa sisi tunacheka etc)
3. Uongozi usio na VISION na kujua watu wanataka nini
4. Kulewa umaarufu.

Unajua hawa jamaa wametokea uswahilini, sasa wakipita huko wanaona wanakubalika kweli kweli, tatizo la uswahilini ni kuwa hata mdhamini hafaidiki nako sana maana VODACOM watumiaji wakubwa na wenye kuiingizia hela hawapo uswahilini.

Shule jamani shule kitu muhimu sana!!

Ila jamaa ni wajanja, maana Manji yupo atawabeba, lakini atawabeba mpaka lini?
 
Ze comedy umaarufu umepungua sana, mie nina sababu kadhaa:

1. Kuishiwa na ubunifu
2. Dharau (mfano masanja anaposema kama hupendi ipotezee, wao wanalipwa sisi tunacheka etc)
3. Uongozi usio na VISION na kujua watu wanataka nini
4. Kulewa umaarufu.

Unajua hawa jamaa wametokea uswahilini, sasa wakipita huko wanaona wanakubalika kweli kweli, tatizo la uswahilini ni kuwa hata mdhamini hafaidiki nako sana maana VODACOM watumiaji wakubwa na wenye kuiingizia hela hawapo uswahilini.

Shule jamani shule kitu muhimu sana!!

Ila jamaa ni wajanja, maana Manji yupo atawabeba, lakini atawabeba mpaka lini?

nakubaliana na wewe kwenye post nzima kasoro hapo ndugu!kwani wewe unaishi dar ya wapi? for my understanding >80% ya dar ni uswahilini.inamaana market capitalization ya vodacom ni hiyo <20% iliyobaki?ndio hao wateja millioni 5 sijui wanaojivunia?

just because unakaa uzunguni usidharau watu wa uswahilini kufikia level hiyo ndugu.

hata kama wanatumia 500 kwa siku that is still too much iwe take (>80% times 500).
sidhani kama hesabu za voda ni <20% times 5,000)

voda hawajafika level ya kuwa-maginalize wateja wao kiasi hicho please withdraw such a statement!
 
Wakuu,

Naomba maana ya neno Uswahilini?

Baada ya hapo Mkuu Kimweri tunaomba utupe "source" ya takwimu hizo hapo juu!


Baba Enock,

Hii ndo healthy debate. View ya uswahilini ni machoni pa mtazamaji. Sinza inaweza kuwa uswahilini au uzunguni.

Ila kusema kweli ni ukweli usiopingika (mawazo yangu) kuwa asilimia kubwa ya watu wenye kipato cha chini ni watumiaji wa TIGO.

Hao walioenda shule kiasi na zaidi huwezi kuwakuta (wengi wao) wakiishi TMK (kwa maana ya Tandika, Yombo na TMK kwenyewe au hata Mbagala.
Manzese, buguruni ni baadhi ya sehemu zinazokuwa regarded kama uswahilini.

Hakuna definition sahihi ya uswahilini ni kutokana na mtazamo wa mwandishi.

Mie ninaishi MBAGALA. Sasa sijui wapi nimesema ninaishi Uzunguni.

Njoo Mbagala hapa rangi tatu utanikuta ndugu yangu na ninaishi uswahilini tu.
 
kazi kweli kweli
maana jamaa wanamwaga data bila kuleta sources.

Mie huwa siangalii ze comedy labda kwa ajali tu niwapo kwenye public area ambapo siwezi kubadili channel
 
HE WHO PAYS THE PIPER CHOOSES THE MUSIC

kwa wengine inaonekana sio comedy kwa anayelipa ndicho akitakacho, simple and clear.
 
Kama wiki mbili hivi zilizopita binti yangu wa miaka 9 aliitwa na mdogo wake wa miaka 5 aende sebuleni kuangalia kipindi cha Komedi Orijini, alimjibu hivi,Nanukuu" Mimi sitaki watu wenyewe hata siwaelewi kabisa siku hizi", mwisho wa kunukuu. Inavyoonekana watu wa rika zote wamewachoka jamaa hawa.
 
Sijawahi kufurahia maonyesho ya Ze Comedy. Sioni kama wanachekesha zaidi ya kunishangaza jinsi wasivyo na ubunifu. Niliwadharau zaidi siku ile walipomkejeli mwanamuziki Banza Stone ambaye ni mgonjwa kwa kusema amefulia. Yule mwigizaji mfupi akawa anaigiza jinsi anavyokohoa. Yale ni maradhi, huwezi kumtania mtu anayeumwa. Hawana utu hata kidogo!
 
Mi nilisha stuka mapema kuwa huu ulikuwa mpango wawajinga fulani kutupotezea muda,hivi wabongo kelele zote hizo hamtaki kuamka?hawa ze comedy ni wajinga coz mnapoteza muda kuwaangalia wakimaliza kipindi wanawaponda badala ya kuwashukuru kwakuchochea UGALI wao,kuliko kuangalia ze comedy ni bora turudi kwenye visa na vituko vya hawa mabwana Comredi Kipepe,Lodi Lofa Dimbwingi,Madenge,Pimbi,Kifimbo cheza na Visa vya Sokomoko!!Ze comedy walifulia b4 hatujawajua runingani,kama huyo Mac Regan alichemka kwenye maigizo ya viwawa ndio ataweza huko,kama wanaweza mcheka aliyefilisika ambaye huenda ndo amewaweka wao pazuri,Vipi bosi wao akipata kilema si watacheka pia?
Amkeni wabongo tuachane na wapuuzi hawa,hawawezi tupotezea muda kijinga!!
 
Nyie hamshangai,huyu SEKIONI anakipaji cha kuchekesha lakini hataki kuonekana kule,sio mjinga huyu kijana ye utasikia sauti yake tuu ,coz alishazisoma alama za nyakati.Kingine naona hii COSOTA haitambui wajibu wake sababu hawa ndio mabingwa wa kukopi kazi za wasanii,sio creative hawa watu,watafute jina lingine na si The Comedy,hivi maigizo ni comedy?sasa ucheshi unaitwaje?hawa wanaigiza tuu,tena mbaya zaidi wanaigiza taarifa ya habari,kama wanapenda fani ya uandishi si waende DSJ,sisi sio watani zao embu watuondolee upuuzi huu,Tido Muhando embu tafuta kipindi cha ku replace hawa mabwana,wanashusha status ya TBC!!
 
sijawahi kufurahia maonyesho ya ze comedy. Sioni kama wanachekesha zaidi ya kunishangaza jinsi wasivyo na ubunifu. Niliwadharau zaidi siku ile walipomkejeli mwanamuziki banza stone ambaye ni mgonjwa kwa kusema amefulia. Yule mwigizaji mfupi akawa anaigiza jinsi anavyokohoa. Yale ni maradhi, huwezi kumtania mtu anayeumwa. Hawana utu hata kidogo!
yah!!,niKweli inauma sana kuona wanawakejeli hata watu wagonjwa,utafikiri wao wana mkataba na mungu.AGRIIIIIIIIIIIIIII!!!!!!!!!!.
 
Last edited:
Kitaalamu Ze Komedi wapo kwenye stage ya mwisho kwenye falsafa ya "Life Cycle". Kwenye hii falsafa ambayo hutumiwa sana na wafanyabiashara wakubwa, kwa kifupi inasema hivi ....biashara yeyote (hapa naamnaisha Ze Komedi) kama ilivyo maisha ya mwanadamu inafuata vielelezo vinne (kuzaliwa (bussiness penetration), kukua (business growth), kukomaa (maturity) na kuzeeka (declining)), bahati mbaya mwanadamu hufa baada ya stage hizo, lakini biashara ikijitambua kwamba sasa imezeeka inaweza kufanya kitu fulani na ikazaliwa upya na kufuata ngazi hizo.
Nao Ze Komedi wapo kwenye "declining" stage, wasipojitambua na ku-rekindle watakufa na kupotea. Great intertainers like Oprah etc they do analyse their business life cycles and that is why they survived decades in the same business. Wanatakiwa waongeze wigo wa ubunifu na kujifunza zaidi, aidha wanunue vichekesho, washirikishe wengine (teaming up), wabadili style, watafute maoni, watumie lugha sanifu, waainishe wateja zao na kujua mahitaji ya wateja na alama za nyakati.

Kwa sasa wanachefua.
 
Duh nakuona unafanya kweli huko hivyo. Pengine huwa sio huru katika kutoa habari za Tanzania na hata vyama vya upinzania. Nyingi za Habari hizo zimejaa bias ile mbaya. inapungukiwa na wabunifu katika ushindani wa Sekta za Habari
 
Back
Top Bottom