Orodha tukufu ya Wanawake maarufu niliowahi kuwahusudu na kuishia kuwala kwa macho

Orodha tukufu ya Wanawake maarufu niliowahi kuwahusudu na kuishia kuwala kwa macho

Kila rijali huwa kuna mwanamke maarufu anayemhusudu ila ndo hivyo huishia kumtafuna kimoyomoyo kutokana na kutokuwepo kwa nafasi ya kuweza kumpata. Ifuatayo ni orodha tukufu ya wanawake maarufu niliowahi kuwala kwa macho. Nitaanzia wale wakongwe hadi hawa wa sasa.

1. Miriam Odemba
Huyu manzi kwa mara ya kwanza nilimuona kwenye tangazo la lotion ambalo jina sikumbuki. Ilikuwa mwaka 1998. Hapo nilikuwa shule ya msingi. Nilipoingia sekondari nikawa simsikii tena.

2. Nora
Huyu mwigizaji nikiwa form one ndo alianza kuvuma akawa anaandikwa sana magazetini. Wakati nikiendelea kumtafuna kwa macho ikatangazwa kuwa kaolewa na mtu aitwaye Ngwizukulu Jilala. Mke wa mtu ni sumu.

3. Sinta
Huyu naye kavuma sana nyakati hizohizo kama za Nora. Msanii Juma Nature alituwakilisha vijana wote kwenye kulifaidi penzi la huyu mtoto mzuri.

4. Kemy
Huyu dada mwigizaji alikuwa anaonekana kama umri umesogea ila mimi haikujalisha. Nilimtaka na huo umri wake.

5. Irene Uwoya
Kwa kumbukumbu zangu mwaka 2004 hadi 2006 nilikuwa bize sana na msuli wa PCM hivyo nikajikuta mambo ya kipuuzi nimepunguza sana. Lakini 2006 kina Uwoya na wenzake walianza kuvuma. Nikajikuta nae nimemtamani ila mchezaji Ndikumana ndo akawa mshindi wa jumla baada ya kumuoa.

6. Wema
Huyu mwanzoni hakunivutia ila alivyoanza kufungasha ile tandam nikanasa.

7. Waziri Kariuki
Huyu mwanamama ni mzuri kinoma. Inagwa umri kanizidi ila anawafunika hadi watoto wa 2000.
Kuna huyu anaitwa lady j Dee huyu manzi Ni mkali sana.

Nampenda bado
 
Kairuki is a really definition of Pisi Kali, gorgeous. Kuna kikao alikua mgeni rasmi aaseee Mungu anaumba,hakika alitumia mda Mwingi kumuumba akiwa amechoka akamalizia kumuumba Dada wa kinyakyusa kukamilisha idadi🤣🤣

2.Mobetooo,ni Hatariii.
Dada wa kinyakyusa 🤣🤣🤣 unamsema dadake Lucas mwashambwa sio???
 
32fe18a1-3969-4edc-8ef8-651aaaf539f8.jpeg
 
Mimi nilitokea kumpenda sana Miss Tanzania wa 2003, Sylvia Bahame.

Kuna dada aliigiza Kaole na kina Dk Cheni wakati ule alikuwa ananivutia sana ila hakuwa maarufu.

Kuna dada pia alikuwa bonge anatangaza Star Tv, nilikuwa nampenda sana ila jina limenitoka.

Wanawake wazuri wapo wengi, angalieni mfano yule mama ambaye ni CEO wa Benjamin Mkapa Foundation.
 
Back
Top Bottom