Orodha ya bidhaa ambazo Serikali inatakiwa izizuie kuingia nchini

Orodha ya bidhaa ambazo Serikali inatakiwa izizuie kuingia nchini

Utani pm # yke mzee mwenzangu

Mm nakubaliana na wewe ufundi wa wa furniture's kote duniani ukiona wanavyotengeneza unaweza usitoe hela

Sema fundi wanazidiana kuna wengine wanajua kuweka uimara na muonekano unakuwa mzuri

Ova
Jamaa kila kitu alichonitengenezea lazima mtu aulize umenunua wapi!
 
Kuna jamaa wachagga nimeona viatu vyao jamaa yangu kavaa sikuamini kama ni made in Tz. Nimeamua naenda kununua soon. Bei kuanzia 45,000
Enzi za utoto kitaani kulikuwa na fundi mmoja anaitwa mfinanga,alikuwa anaunda viatu vizuri sana ...soli kali,ngozi badaye akaachana na shuguli hiyo kabisa
Hapo kwake tulipiga sana deiwaka za kushona ndala na kuweka viraka kwenye viatu
Najiulizaga hao wanashindwa nn kujitanua wigo awe na kijikiwanda

Ova
 
Kuna jamaa wachagga nimeona viatu vyao jamaa yangu kavaa sikuamini kama ni made in Tz. Nimeamua naenda kununua soon. Bei kuanzia 45,000
Huyo siyo ouwiso wa salasala

Ova
 
Enzi za utoto kitaani kulikuwa na fundi mmoja anaitwa mfinanga,alikuwa anaunda viatu vizuri sana ...soli kali,ngozi badaye akaachana na shuguli hiyo kabisa
Hapo kwake tulipiga sana deiwaka za kushona ndala na kuweka viraka kwenye viatu
Najiulizaga hao wanashindwa nn kujitanua wigo awe na kijikiwanda

Ova
Kuna jamaa enzi za sekondari nishachonga English boot hapo mtaa wa Sekenke Kinondoni Manyanya. Huwezi amini kama ya Bongo
 
kazi za mbao ni rahisi sana Tatizo ni machine mafundi wetu hawana! na uzuri wa mchine za mbao unakuta machine moja ina operesheni 4, 6 serekali inge ondoa ushuru kwa 100% kwenye machine ndogo ndogo na zakati! au ingesaidia kutengeneza karakana za kisasa kwa vijana wa vyuo vya ufundi!
zinge inua ubunifu!
Ah basi tu mafundi wetu hawataki kujiongeza
Tatizo linakuja kwwnye uimara

Ova
 
Tatizo mafundi wetu hawajielewi hawana professionalism kbsa wameendekeza sana uswahili, usipokuwa makini kabati tu utajengewa kwa miezi hta nane!...ndio maana watu wengi hawataki usumbufu wanaamua kwenda dukani kununua furniture za mchina.

Ukiunda mazingira wezeshi ya ushindani wa ndani magugu yatajitenga na ngano. Mafundi wenye weledi na nidhamu ya kazi watapata wateja na wale mizinguo watapotea ndo ushindani wa biashara. Sasa hata wale wazuri wachache hawaonekani sababu wanafichwa na ushindani wa nje.

Shida na mafundi wetu upuuzi ni mwingi. Mtu anaweza lipa fundi ila akazungushwa hadi akajuta kuingia nae mkataba wa kazi.
 
Discount centre sasa hivi furniture zao wanatengeneza hapa hapa na zinaridhisha. Kuna fundi juma wako vizuri balaa. Nina fundi wangu ni balaa kazi yangu natoa picha Google maps anatoa kitu kikali kuliko cha kwenye picha kwa material unayotaka wewe.

Mimi kuna mmoja nilionyeshwa products zake ni hatari aisee na bei zao ni nafuu. Hawawezi kuonekana kama mazingira ya ushindani wa biashara sio rafiki kwao.
 
Ni ajabu hakika. Akili zimelala kabisa.

Ila kwa niijuavyo bongo na wabongo wenyewe, mtu yupo radhi kununua kitu kwa bei kubwa na poor quality cha nje kuliko kizuri kwa bei poa cha ndani. Utasikia ninunue meza ya fundi Juma mimi kwa laki2 wakati shoppers zipo za Uturuki ilhali ya Uturuki ni laki5 and no any better than Juma's.
Nilienda pale Mlimani city nikakuta Sofa seats 7pc zinauzwa milioni kumi na laki kadhaa...nikasema Hiiiii (kwa sauti ya Mwanakwenda)
 
Ah basi tu mafundi wetu hawataki kujiongeza
Tatizo linakuja kwwnye uimara

Ova
mkuu katika hali ya kawaida fundi ukimuambia atafute 20m anunue machine au ata 10 au 8 ni kazi nzito sana! ila hakuna uwekezaji mwepesi kama kuwekeza kwenye machine za bidhaa za mbao na zina faida kubwa sana sana uimara ni chaguo la mteja! sio lazima uwe fundi mtu yoyote anaweza anzisha factory ya kuzalisha bidhaa za mbao!
 
Mimi sioni haja ya kuzuia hizo bidhaa maana sasa soko linataka bidhaa zilizotayari na tofauti kwa mtumiaji Ili aweze kuchagua sasa hao wanatengeneza kwanini hawatengenezi bidhaa zilizotayari? Tatizo ni ujuzi hawana kabisa na mashine hazipo hivyo Kama kweli wanataka kuzuia bidhaa basi ndani ya miaka mitano wangeruhusu mashine hizo bila kodi baada ya hapo hizo bidhaa zingetoweka zenyewe, sasa sokoni hatuna bidhaa so tunazihitaji sana.
Hapo kwenye kodi Hapo.
 
Nilienda pale Mlimani city nikakuta Sofa seats 7pc zinauzwa milioni kumi na laki kadhaa...nikasema Hiiiii (kwa sauti ya Mwanakwenda)
Kuna siku nilikutana na mama m1 ni wazir machachar sana ananunua furniture za nyumban kwake mahali 24m jumla ilikua..mikochi ya leather mibayaaaaa...nkasema dah.kwel usipokua na hela unakua unajua vtu vzur sana...
 
mkuu katika hali ya kawaida fundi ukimuambia atafute 20m anunue machine au ata 10 au 8 ni kazi nzito sana! ila hakuna uwekezaji mwepesi kama kuwekeza kwenye machine za bidhaa za mbao na zina faida kubwa sana sana uimara ni chaguo la mteja! sio lazima uwe fundi mtu yoyote anaweza anzisha factory ya kuzalisha bidhaa za mbao!
Utengenezaji wa masofa unafikiri inahitaji mambo ya mashine nyingi mambo madogo
Kikubwa kwenye utengenezaji uimara unatokana na ugongaji wa mbao tu

Kama alikuwa Waziri basi ujue hizo hela alizokuwa ananunulia hayo makochi zilitokana na kodi yako!!! Hawa jamaa wananunuliwa na serikali mpaka makochi ya nyumbani!.
 
mkuu katika hali ya kawaida fundi ukimuambia atafute 20m anunue machine au ata 10 au 8 ni kazi nzito sana! ila hakuna uwekezaji mwepesi kama kuwekeza kwenye machine za bidhaa za mbao na zina faida kubwa sana sana uimara ni chaguo la mteja! sio lazima uwe fundi mtu yoyote anaweza anzisha factory ya kuzalisha bidhaa za mbao!
Kitambo sana nlikuwaga kwenye chuo kimoja cha mafunzo,nje lkn huko walikuwa na kitengo cha mambo ya mbao,jamaa wanatengeneza masofa hTari walikuwa wanatumia mpaka mbao inayotokana na mnazi
Walikuwa wanatumia marine boards,mbao 1×6,maboxxx,masponchi,vitambaa etc
Sofa ikitoka hapo huwezi amini

Msumeno wanatumia wa mashine na wanatumia mashine ya ku round

Jamaa walikuwa wanapiga kazi balaa

Sofa ikitoka hapo ahh lazima ukubali

Ova
 
Utengenezaji wa masofa unafikiri inahitaji mambo ya mashine nyingi mambo madogo
Kikubwa kwenye utengenezaji uimara unatokana na ugongaji wa mbao tu

Ova
kabisa mkuu na kitambaa imara tu! karibia maduka yote wana karakana za kutengenezea hapa hapa na ukiituta dukani utauzia 20 na zaidi utambiwa hii ni kutoka Uturuki au nje kumbe wametengeneza hapa hapa!!
soko hili ni kubwa sana ni mtaji tu wala halihitaji akili kubwa sana soko lake ni kubwa sana sana na la uhakika sio rahisi mtu aliye anzisha akiwa na mtaji akaanguka ni ngumu sana maana kazi ni nyingi sana!
na mafundi ndio hawa hawa wa kwetu!
yule mjane wa mengi mbona alifanya vizuri sana sana sijui siku hizi yupo wapi na alikuwa ana tengenezea hapa hapa ila ukiona una hisi zimetoka UK
 
Bei zake sasa za masofa alikuwa anauza kufuru
Wakina RRONDO Ndy wanaziweza😂

Ova
 
Back
Top Bottom