Kwa hiyo tunakubaliana kwamba kumbe serikali inapendelea hiyo mikoa yenu na kutenga mikoa yetu hasa Mbeya?
Hata mtutenge tunawakimbiza hivyo hivyo.
Hakuna mkoa unaotengwa kama mwanza mzee hata serkali inajua! Mwanza inapaswa kufukuzana na Dar miaka mingi! Na ukija mwanza na ukawa hakuna jicho la wivu kutembea utaamini! Investment za watu mitaani nyumba kali na innovation ni nyingi sana! Mi niko Dar kitambo ila mwanza respect sana! Tuache wivu usio na tija mji unaendelezwa na wenyeji na wageni kwa kushirikiana!
Saizi ukiangalia JPM bridge ikishaisha mji utachangamka zaidi kutokea busisi kwenda sengerema na serkali imeshapima viwanja maeneo yote mpaka sengerema! Means mtu ataishi sengerema na kufanya kazi upande wa pili!
Pia kuna mgodi mkubwa wa dhahabu Nyanzaga maeneo ya wilaya ya sengerema itaukuza sana mji wa mwanza!
Kwa ujumla future ya mwanza ni kubwa kwa kuwa jamii ya wasukuma pia ni hard working nasema hivo kwasababu saizi vijiji takribani vyote vinageuka kuwa mji midogo na watu wanajenga nyumba za kisasa kila kukicha!
Mfano Mhungumalwa,kasamwa nk!
Ukitaka kujua pia mwanza ni second super power baada ya Dar nenda kaulizie wataje wa mashirika ya ndege kwa local route watakwambia watu ni wengi sana ukanda huo wanasafiri!
Ukija hapo bandarini magari yakifika bandari ya Dar ukitoa magari yanayoenda transit,Kwa yale yanayobaki nchi mengi yanabaki Dar na mkoa unaofuta kwa magari kubaki nchini ni mwanza!
Mwanza pia imeshatoka kwenye level ya mkoa wetu watu wa sehemu fulani kama huko Mbeya ,Mfano wawekezaji na watu wenye biashara mwanza wanatokea mikoa yote nchini pale utamkuta Msukuma,mkurya mhaya ,mchaga nk!
Kwa ujumla mwanza ni potential sana na kwa sasa ndo mji wa pili kwa watu kuhamia kutoka maeneo mengine baada ya Dar!