Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Kabla ulipaswa uweke vigezo vyote vinavyotimika/takiwa kwa eneo au mji kuwa Manispaa.(Kisiasa,kijamii,kiuchumi,kijiografia nk)
Hapo ungesaidia wachangiaji..wewe umeleta uzi kwa kutumia kipimo cha macho yako.
 
kuna wilaya ina itwa mwanga wanahadhi ya mji mdogo pale tambarare ila kiukweli ni kama kakijiji naenjoy kufika na kukaa kwakua ni home ila sio siri hata hadhi ya mji mdogo haipo labda ilikuja kwa heshima ya baadhi ya viongozi na wadau wa chama wenye heshma.....
 
Lindi haina hadhi kabsa hii manispaa itaifishwe
 
Kuhusu umeme hapa nawapa kongole, pia miundombimu ya barabara na yenyewe sio haba, huu mradi unaoendelea ukikamilika mtatisha kidogo
Mimi siishi Sumbawanga ila nilikuja huko mwezi wa 6 aseeh huo mji ni tofauti sana na wengi wanavyoweza kudhani. Naona maendeleo yapo sana tu ila mapungufu hayakosekani kama maeneo ya Mandela haikupaswa kuwa vile kabisa. Nikaambiwa pia kuna hospitali mpya inajengwa maeneo ya Mtimbwa.

Sifahamu na hujanambia kuhusu huduma ya maji ikoje
 
Sijajua mtaani kupoje, ila kwenye Lodge niliyopo sijakutana na changamoto ya maji mwezi wa pili sasa.

lakini pia utamaduni wao wa namna wanavyojenga nyumba zao kidogo unaharibu muonekano wa mji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…