Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Orodha ya Miji yenye hadhi isiyostahili

Kumekuwepo na mjadala kuhusu Majiji.

Ukweli ni kwamba sio Majiji tu ambapo yapo yenye hadhi hiyo ilihali kiuhalisia ilipaswa yawe manispaa Tu.

Leo nakupa orodha ya manispaa zisizostahili hadhi hiyo.

1. Lindi
2. Shinyanga
3. Tabora
3. Singida
5. Kigoma
6. Songea
7. Musoma
8. Bukoba

Manispaa hizo kimiundombinu na maendeleo ya mtu mmoja mmoja bado Sana. Mfano Shinyanga nilipofika nilibak mdomo wazi.

Taja manispaa zingine
Shinyanga baiskeli ndiyo usafiri 😀😀
 
Mi kila nikija Sumbawanga kuna samaki fulani ni mtamu anaitwa Kuhe ila anauzwa bei kubwa kiasi. Siwezi acha kumla aseeh. Wanamuita kuku wa ziwani.
Kwa mara ya kwanza nimefika kipili ilikua 2005 ila Kirando sikuwahi kufika.

Umenikumbusha mbali aseeh. Nataka kufanya tour nyingine nifike Lupita Island
Duh kweli jf kuna wazee! Mimi kipindi hicho hata kutembea sijaanza
 
Labda utazame hii video kuhusu Bukoba na utaona waliioita Bukoba municipality miaka ya 90 hawakuwa wajinga....

Huu mji una busy Airport, uwanja mzr wa kapeti kaitaba, bandari ya pili kwa ukubwa kanda ya ziwa, hotel za nyota 3 kibao, mtandao mkubwa wa Barabara za lami na kwa kanda ya ziwa Bukoba ndo mji wa pili baada ya mwanza kwa idadi ya maghorofa ( sensa 2022)

Miradi inayoendelea ni ujenzi wa Barabara ya njia nne km 5, stendi ndogo ya mjini kati, stendi kubwa, chuo kikuu nk


View: https://youtu.be/rBYKFm9U19w?si=h1GCv0cpy0sG_sQN

Fuatilia vzr historia, bukoba ilitangazwa kuwa manispaa mwaka 2005, b4 ilikuwa ni halmashauri ya mji
 
Kwani kuna shida gani baiskeli kuwa usafiri? Si ndio vizuri kuhakikisha kuwa energy efficient transport means?
😀😀😀Nikweli haileti air pollution ila kwa speed ya Baiskeli,inasababisha na maendeleo ya mtu mmoja mmjo kuwa na speed hiyo hiyo,ndiyo maana mleta Uzi amedisqualify Shy town kuwa Municipal
 
😀😀😀Nikweli haileti air pollution ila kwa speed ya Baiskeli,inasababisha na maendeleo ya mtu mmoja mmjo kuwa na speed hiyo hiyo,ndiyo maana mleta Uzi amedisqualify Shy town kuwa Municipal
Umeangalia upande mmoja tu. Baiskeli inakufanya usipate magonjwa na hivyo automatically unakuwa tajiri wa afya na kiuchumi. Fikiria nje ya box mkuu
 
Back
Top Bottom