BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Msaada,
Kwanza kabisa, mimi ni muumini wa dini ya Kiisilamu, lakini naisoma Biblia hatua kwa hatu, Mistari ifuatayo imenichanganya sana kunako swala la Ubatizo. Inaaminika kwamba kila mtu huzaliwa akiwa ni muislamu hadi pale atapobatizwa ndio atakuwa Mkristo safi. Sasa ubatizaji nimeokutana nao katika biblia naona umegawanyika vifungu vitatu na sielewi kipi ni sahihi kufuatwa.
MATHAYO 3:11
Kweli mimi ''nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba'' bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; ''yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.''
MARKO 1:8
Mimi ''niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.''
LUKA 3:16
Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi ''nawabatiza kwa maji;' lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; ''yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto''
YOHANA 1:33
Wala mimi sikumjua; lakini ''yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, ''Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, ''huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.''
.................
Ubatizo wa Yohana ni "maji" , ubatizo wa yesu ni "roho mtakatifu na moto". Kwahiyo Yohana alibatiza watu katika maji ya mto kama yordani (maji mengi) lakini yesu na wanawafunzi wake walibatiza bila maji:
Navyofahamu "ubatizo" ni neno lenye asili ya kigiriki maana yake: "kuzama mwili wote"
kwahiyo;
1) Ubatizo wa maji: kuzama katika maji mwili wote (full immersed in water)
2) Ubatizo wa moto; ulipaswa kuwa "kuzama mwili wote katika moto unaowaka"
3) Ubatizo wa roho mtakatifu ulipaswa kuwa "kumezwa mwili wote na huyu roho mtakatifu"
..............
1) ubatizo wa maji umethibiti kutumiwa na Yohana na ata Yesu amebatizwa na Yohana kwa ubatizo huo katika mto yordani pia wakristo ata sasa wanatumia ubatizo huo "tunashuhudia"
2) ubatizo wa moto haijathibiti kutumika na yeyote, mfano wa ubatizo huu ulipaswa kuwa kama Ibrahimu katika kisa cha kuchomwa moto na Nimrod kwa kosa la kuvunja masanamu yao akatoka salama bila kuungua.
3) Ubatizo wa roho mtakatifu, haijathibiti kutumika (kama maana halisi ya neno "ubatizo") ubatizo huu ulipaswa kuwa kama kisa cha nabii Yona (Yunus) kumezwa na samaki alafu kumtema akiwa hai basi roho mtakatifu katika ubatizo huu alitakiwa kuwameza watu, na kuwatema wakiwa hai.
.........
Sasa tumeona
1) Ubatizo wa Yohana -- kutumia maji (confirmed)
2) Yesu na wanafunzi wake walibatiza bila maji lakini haikuoneshwa namna walivyobatiza watu--kivipi (hidden)
3) Swali linabaki sasa kujua "ubatizo aliofundisha paulo" --ni upi ??
Rejea hoja: "ubatizo wa Yohana na ubatizo wa Yesu" swali je Paulo kafundisha ubatizo gani ? je ndugu zetu wakristo wanafuata ubatizo gani ?