Orodha ya Mistari iliyo nichanganya kwenye Biblia takatifu kuhusu Ubatizo

Mkuu, tembelea na hivo vifungu nimevyokuwekea hapo kuhusu ubatizo wa MOTO
 
Umekubali kwamba sikuzaliwa muislamu?
 
Tunaomba mistari inayochanganya kuhusu matumizi ya pombe
 
Umekubali kwamba sikuzaliwa muislamu?
Lakini mbona Yesu (a.s.) hakurithi dhambi ya asili hata uhitajike kwake ubatizo huo wa Yohana. (Tazama Kumbukumbu la Torati 24:16 na Ezekieli 18:20). Na kwa kweli hiki pekee ni kigezo tosha kinachomvua Yesu (a.s.) na dhana ya kubatizwa na Yohana.

Ndugu usipobatizwa bado unakuwa ni Muislamu.
 
Hivi nawewe unakubali kabisa kuwa uislam ulikuwepo kabla ya watu?

Huwa mnanichanganya hapo tu, kwasababu ushahidi wa kihistoria unaonesha wazi kuwa uislamu umekuja recently
Turudi kwenye hoja ndugu, vifungu hivyo vya ubatizo wa Maji, ubatizo wa roho mtakatifu na ubatizo wa moto kipi kinatakiwa kufuatwa
 
Itakuchanganya sana...
Mambo mengine muachie ALLAH SUBHANAHU WA TAAALA
Yale yanayopaswa kumuachia tayari ameyaficha na wala hatuyajui, ila kwa haya aliyotufunulia ni vyema kuyafafanu. Unaelewa vipi kuhusu ubatizo wa MOTO, MAJI NA ROHO MTAKATIFU
 
Yale yanayopaswa kumuachia tayari ameyaficha na wala hatuyajui, ila kwa haya aliyotufunulia ni vyema kuyafafanu. Unaelewa vipi kuhusu ubatizo wa MOTO, MAJI NA ROHO MTAKATIFU
Tunayajua ila maisha mazima sio kwa uwezo wetu, ni kwa uwezo wake...tunamtegemea.
Ubatizo wa roho mtakatifu ni kujawa na roho wa Mungu aliyemtakatifu ndani yako... na hio haikuwako kabla ya Yesu( nafikiri ndio maana yesu alibatizwa kwa maji)
Pia maji yana maana nyingi sana juu ya mtu.. ubatizo wa Roho mtakatifu ilianza baada ya Yesu kufa

Matendo ya mitume 2 : 1 - 4
Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
 
Ahsante kwa ufafnuzi lakini bado sijapata kuona wapi Yesu au wafuase wake wamebatizwa kwa MOTO na ROHO MTAKATIFU kama vifungu nilivyo vitoa vinavyo ainisha kwamba atabatiza kwa MOTO
 
Iamini injili acha kucelewa
 
Iko hivi, vitabu vyote watu wanavyoviita vitakatifu vimeandikwa katika codes, na hizi codes sio rahisi kuzi.break kama ulivyosoma, mfano mdogo ni sheria. Huwezi kuijua sheria kama si mwanasheria. Vinginevyo utatafsiri tofauti vifungu vya sheria
 
Kwa hiyo tunafanyaje? ni upi muongozo
 
Sasa dhumuni la kubatizwa ni lipi kama hukuzaliwa Muislamu. Naomba unifahamishe
Dhumuni la kubatizwa ni kuondolewa dhambi ya asili tuliyoirithi kutoka kwa Adamu na Hawa. Kwa mantiki hii ikiwa binadamu huzaliwa akiwa ni Muislamu basi uislamu ndio dhambi yenyewe ya asili. Basi nyinyi mwazaliwa dhambini na kufa dhambini. Poleni
 
Ahsante ndugu, na vipi kuhusu ubatizo wa MOTO
 
Anzia kwenye vitabu vimeandikwa na waandishi watatu tofauti kwaiyo kila mmoja ipo jinsi anavyoelezea jambo lilelile ila maneno yaliyotumika yanaweza yasifanane hapo wewe shika lengo kuu la kinachowasilishwa apo
Pili usipende kuyatafasiri maneno ya biblia kwa kusoma aya moja fuata mfululizo wa sura nzima imebeba fundisho gani (yona hakumezwa na samaki ili kubatizwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…