[mention]Undava King [/mention] Mkuu nimeota nipo naiingia chumba cha mtihani wa form 4 ila sikujisomea kama miezi 6 hivi ya kujiandaa na huo mtihani, kwahyo nikawa napanga kukaa na rafiki yangu ili niigilizie, tukakaa na rafiki yangu lakini sikuiigilizia, walimu wakabana nikaenda home kupumzika baada ya mtihani, badae napata taarifa kuwa kuwa kuna mafuriko mtaa wa pili na mdogo wangu anakuja home kunisimulia namna alivyonusurika kufa kwenye mafuriko hayo na alinihadithia jinsi watu mbalimbali wamekufa ila yeye kapona.

Ila ndoto hiyo ikawa inanifanya kujuta kufanya mtihani bila kusoma miezi 6 inanisuta, na najutia kwanini sikujiandaa, mpaka nastuka usingizini nashangaa ile roho ya kujuta kufanya mtihani bila kujiandaa nikiwa nayo, mpka akili zimerudia ndo nkatambua kuwa mimi si mwanafunzi na nilishafanya mitihani miaka ya nyuma sana.


Hii kujutia kufanya mtihani bila kujisomea miezi 6 ndo imenitisha mpka sasa roho inaniuuma kisa huo mtihani na mm si mwanafunzi wa aina yoyote.


Nini maana ya hii ndoto?

natanguliza shukrani
 
Kuna kazi ya maana niliomba kwenye taasisi Fulani sasa nimeota nimeikosa na nimedhaika Sana aisee

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Una sintofahamu juu ya maamuzi yako mwenyewe juu ya wapi uanzie kutoka katika comfort zone, ndoto inajaribu kukwambia usiendelee kukwepa majukumu.
 
Kuna kazi ya maana niliomba kwenye taasisi Fulani sasa nimeota nimeikosa na nimedhaika Sana aisee

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Unapaswa 'kujiamini' hivyo hakikisha unaongeza uwezo wako wa kujithamini na kutojidharau kuwa uwezi. Pia kwa upande mwingine ni ishara ya kufungika kwa mlango mmoja na kufunguka kwa mlango mwingine hivyo get ready kwa fursa iliyo mbele yako.
 
Bado haujawa tiyari kukabiliana na uhalisia wa maisha yako kwa kuuvaa ujasiri wa kuzikabili changamoto na magumu yake.
 
mbona najitahidi kuizikabili ila mamb hayajakaa sawa na matatizo hayo bado ni nayo
Ndiyo maana ya ndoto za namna hiyo umtokea mtu mara kwa mara pindi anapokuwa akikabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha mpaka pale anapofanikiwa ndipo ukoma, kumaanisha kuwa umefahulu kuvuka hatua hiyo ya maisha.

Hivyo ni kawaida tu Mkuu Nshomile endelea kupambana pasipo kuchoka utafanikiwa.(kitendo cha kuota mafuriko(misukosuko) kuwa yameua wengine na mdogo wako akabaki ni ishara kuwa utafanikiwa licha ya magumu unayopitia)
 
Ndoto hiyo ilikuwa inakupa tahadhari kuondokana na tabia isiyofaa inayoweza kukuangamiza au hatarishi kiafya au kujihusisha na watu wasiofaa katika mahusiano au maisha yako.
 
Inaonekana unapenda sana kuangalia movie za kivita mkuu
 
Mkuu, acha kabisa. Mimi vita ndio huwa ndoto zangu, hata sielewi ni nini yani. Huwa naota vita, yaani tumevamiwa, na wanajeshi huwa wamevaa kabisa nguo za kijeshi. Wanaingia mtaani, wanaanza kusaka watu. Mi nikiwa mmoja,wao, basi tunajificha. Mara nyingine wanatuona, nikikimbia nakutana nao, risasi zinakuwa zinapigwa. Ndoto zote za vita huwa zinakuwa mida ya jioni, yani kama saa 12 hivi kuelekea saa moja maana kunakuwaga hakuna jua. Juzijuzi tu, nimeota vita tena. Ndoto imeishia nimekmbia kuwakimbia wanajeshi, kumbe nilikokimbilia ndio nikakutana nao wawili. Mmoja akanielekezea bunduki, ile anataka tu kunifyatulia nikashtuka ghafla. Nilivyoshtuka nikakuta nwili wote unatetemeka, moyo unaenda mbio.
Sijui ndoto za vita huwa zina maana gani maana kwangu hiwa zinajirudia mara kwa mara.
 
Ninaomba tafsiri ya ndoto hii.

Tulikua tunakunywa chai na ndugu zangu akiwemo mama yangu..pembeni kuna kitu kama gogo hivi..sasa akaja ndugu yangu akalishika lile gogo.Kumbe ni Joka kubwa mno..likivyoamka tukakimbia..ila likavingirisha mama pale..hapo hapo nikastuka.

Msaada please nmeota leo leo hii.
 
Msaada ndugu Undava King: kuna binti alikuwa damu wangu lakini tulikwisha achana kitambo tuu tokea mwaka jana lakini tokea mwezi wa pili mwaka huu najikuta namuota mara kwa mara kwamba anakuja kwangu kuniomba msamaha
Hii imekaaje??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…