Wasaaalamu nyote humu
Niende moja kwa moja katika mada tajwa, hii ni ndoto niliiota siku tano zimepita.
Niliamka usiku mida ya saa saba, nikaanza kufanya shughuli zangu binafsi katika kompyuta yangu, ilipowadia SAA kumi na mbili na dk 38 asubuhi niliamua kujilaza kidogo ili niamke saa mbili asubuhi niendelee na ratiba zangu, Cha ajabu niliamka saa moja na dk 13 asubuhi.
Nilivyolala sikuchukua hata sekunde, nikamuona mpenzi wangu mbele yangu, akiwa uchi kabisa, akipita, Mimi nikiwa nimesimama kwenye mlango, nilimuita kwa jina lake hakuitika ila alizidi kutembea na kuelekea mbele, nilimfata nyuma nijue anaenda wapi, baada ya dakika chache akaingia katika nyumba iliyoezekwa kwa nyasi na mlangoni kulikuwa na vijana wawili wa kimasai wamesimama wakiwa wameshika mikuki na Mimi niliingia ndani, nyuma yangu wakaja vijana wawili wa kimasai na mtu mwingine mmoja ambaye ni kama alikuwa ananifuata Mimi, na alikuwa analazimisha kuingia ndani, alivyoingia alipigwa kitu kichwani akaanguka chini, wale vijana wakaondoka zao, baadae kidogo nikawaona wazee wawili wakimasai wamekaa kwenye makochi yasiyo na mito yake, baada ya muda nikahisi niko kitandani kwangu na yule mpenzi wangu akiwa amenishika kiuno changu, tukiwa hatujageukiana, kwa maana ya yeye yuko ukutani anatizama kisogo changu na mkono kiunoni, nikamsikia akiniambia "haya fungua macho uende, nimeshamaliza" ila nikataka kumuuliza umemaliza nini?
Sikuweza, mdomo mzito ila kichwani najua nataka nimuulize nini! Basi nikafumbua macho kweli nikiwa chumbani kwangu ila kiuno bado kilikuwa kinahisi kuna mkono wake, nilivyofumbua macho akili akanambia rudi muulize amemaliza nini?
Nikafumba macho, nikamuhisi kabisa bado mpenzi wangu yupo nyuma yangu amenishika kiuno, nikamsikia ananiambia umerudi? Haya basi fungua macho uende, hapa haturuhusiwi kuzungumza!
Nikajitahidi kunyoosha kidole kuonesha "Nina jambo moja tu" ila sikufanikiwa. Ikanibidi nifungue macho kweli na bado nilihisi yuko nyuma yangu na nilihisi pumzi zake nyuma yangu, hiyo ni asubuhi saa moja na dk 13 niliangalia saa yangu.
Hii ndoto inanipa wakati mgumu wa kuielewa. Mwenye kufahamu maana yake anijuze.
Kitu kingine, mie ni mtu ambaye nikisema nalala muda huu na nitaamka muda huu, hata nisipoweka alarm ni lazima niamke muda husika ama pungufu ya dk 2/3. Sikuzote.