Mimi naota sana ndoto lakini ikifika asubuhi sikumbuki nimeota nini?
 
Ukiota ndoto umeenda chooni, tafadhali usije ukathubutu kukunya. Maana asubuhi lazima utakuta limenata kwenye shuka...🙄🙄
 
Mmmh inasikitisha sana. Hata mm kwa kiasi fulani naamini ndoto ingawa napuuzia . Nilishawahi kuomba kitu kwa uchungu.nikimuomba Mungu anipe jibu. Siku hiyo nilishinda nalia kanisani haikuwa siku ya jpili so nilikuta kanisa liko wazi iliidi nipeleke lawama zangu altare .
Nilimaliza masaa ma 3nahisi niliongea kwa hasira nikamwambia Mungu. Leo hii naomba jibu ukichelewa nahisi ntapasuka.

Nikarudi kwangu nikalala. Saa 11 alfajiri mama ananipigia. Mwanangu nimeota hivi na hivi na ndoto imejirudia. Moja kwa moja nikajua Mungu jibu kapitisha kwa mama. Saa 7:30 nikapiga siku kuhakikisha. Sikuamini jibu nililopewa. Kama mama alivyoota ndivyo ilivyokuwa. Hii sitokaa niisahau..............wewe fulani uishi miaka mingi.
 
Si ungeni PM jamani tushee mawazo.

Mi huwa nikiamka usiku nikiwa sina usingizi nasomaga kitabu.

#YNWA
 
Asante.

Nitaishia miaka 100.

#YNWA
 
Naomba kuelekezwa hii ndoto maana yake,nimeota tunahamisha jeneza la baba yetu sehem aliyozikwa awali ambayo ilikua ni sehemu za milimani tunahamisha sehemu ya tambarare,wakati tunahamisha jeneza linadondosha uchafu,cha ajabu jeneza lilitolewa Kwa pembeni mwa kaburi na ni safi kama halijatumika ila mwili upo ndani,mwenye uelewa wa tafsir
 
Wakuu wacha niende moja kwa moja kwenye mada,

Leo nimeota nimekutana na jamaa ambaye amefariki kitambo nikasalimiana naye na kupeana mikono kabisa, nikaendelea mbele nikakuta mto una mamba sana pembeni kuna utelezi sana nikaghaili kuvuka nikapandisha kilima kwa kutambaa kuogopa kuteleza kudondokea mtoni.

Anaejua haya mambo jamani naomba anisaidie.

Karibuni.
 
Wakuu wa jukwaa Hili wasalaam kwenu,
Leo mida ya saa nane niliposhtuka kutoka usingizini nimeota vitu viwili

Cha kwanza
Nimeota nimepima ukimwi na majibu yamekuja sina ukimwi(negative)

Cha pili
Nimeota nimefanya mtihani kwa combi ya PCB na matokeo yamekuwa hivi
Physics =D
Chemistry=C
Biology=C
Ikiwa na maana matokeo ni division two ya 10 , kwa wale waliosoma miaka ya nyuma Kidogo (25 iliyopita) , sijui sasa wanahesabu vipi.
Lakini hapo nyuma nilikuwa nikiota nafeli sana mitihani , na nikilichanganya Hili katika biashara zangu Nina kama miezi miwili sasa sifanyi biashara maana zinaniendea vibaya sana. Lakini Leo nashangaa kuota ufaulu huo. Nina zaidi ya miaka kama nane hivi nikiota ndoto za kufeli mitihani , ila Leo nimeota ya kufaulu mtihani.

Dhumuni la Uzi huu nikuomba tafsiri ya haya mambo kwa wale wajuzi wa ndoto.

Natunguliza heshima na shukrani na pia Naamin nitapata tafsiri hizi
Asanteni wote
 
Ulishapata majibu? Nilisaidie
 
Leo nimeota kwamba tumeenda field na zitto Kabwe,wenyewe wakatungulia mbele sisi tukabaki nyuma muda kidogo dereva wake anarudi bila gari,anatueleza walipofika mbele wamepata ajali zitto ameumia lakini cha ajabu yeye hajaumia hata tone.

Basi wote tukakimbia kwenda kuangalia tukakuta Jamaa amelala chini amepasuka kifua chote na tumboni amechanika utumbo upon nje lakini bado anaona na kupumua.

Kile kitendo cha watu kumuinua kutoka chini,nikaona macho yake yote ananitazama Mimi vile alivyokuwa ananiangalia huku anatoa machozi ghafla ndoto ikakata na nikasituka.

Nilitaka niandike ile asubuhi kama Uzi lakini nikaona sio ungwana,ninaitafakari ndoto hiyo hadi sasa pasipo majibu.wataalamu wa haya mambo nisaidieni.
 
Wakuu kuota umetokewa na jini ambalo limekuja mfumo wa binadamu yaani mwanamke akiwa na watoto watatu wamenitokea chooni wakati natoka mlangoni na alikua anataka hela na nikampatia hela ya noti akanirudishia chenchi, na tukaongoza kuondoka na kupiga story na kuelekea nisipokumbuka,hi ina maanisha nin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…