Orodha ya Walipa Kodi Wakubwa 40 - Taasisi za Serikali

Hapa naomba ufafanuzi,unamaanisha hizo taasisi ulizozitaja ndo zimelipa kodi,au wafanyakazi wa taasisi hizo wanakatwa makato ya kodi afu ndo zinatajwa kwa jina la mwajiri wao(Taasisi)?
Mlipa kodi natamani awe ni yule anayevuja jasho lake na kukatwa kodi ndiye atajwe ,badala ya usanii huu
kodi anakatwa mwingine heshima anapata mwingine.
 

I can understand, bado kuna sigara, bia, migodi n.k that list is not logical...magereza wanalipa kodi gani?? ka biashara ipi??
 
sasa Air Tanzania wanalipa kodi kwa ndege zipi walizonazo?
na TRA nao kumbe walipa kodi?
 
Hii list ina walakini sijaona

1. CRDB

2. Tanzania brewaries

3. Migodi ya dhahabu

4. Vodacom

5. NMB

6. Sigara

7. Cocacola

9. Pepsi

10. Azam

..............
 
Mtoa mada hivi umesoma wapi wewe???myb ukisema elimu yako sitakulaumu
 
Hivi source of income ya Magereza ni ipi ndugu zangu mpaka wawe walipa kodi wazuri?..au ndo kutoa pesa mfuko huu then unarudishia mfuko mwingine kwa kuipa jina jingine
 
Hiyo list sio walipaji wazuri wa kodi itakuwa walipaji wazuri wa pension or the like,

naona mtoa uzi anaongelea PAYE na withholding tax may be in term of public institutions na naamini ameamua tu kutoa mtazamo wake
 
Cha ajabu inakuwaje Vibenki kama Pastal bank(12), TIB(16) na Twiga bancorp(18) wapo ndani lakini benki kama CRDB,NBC,NMB,EXIM hawapo? It is a shame list
 
Hapa changa la macho mbona makampuni binafsi hayapo.... TBL, TCC vodacom na mengine au ndo misamaha ya kodi?
 
Wakuu ni jambo jema kuelewa title na maswali makuu ya mtoa mada;

1. Orodha iliyotolewa ni ya walipa kodi wakubwa ikihusisha taasisi za serikali, wizara na mashirika ya serikali tu. Haihusishi taasisi au kampuni binafsi ambazo nitatoa uzi mwingine.
2. Hii ina maana taasisi zote zinamilikiwa na serikali au kwa kiasi kikubwa na serikali.
3. Nilichoomba ni mchango wa waelewa hii inaweza kuwa na maana gani. serikali inakusanya mapato yake kupitia kodi mbalimbali kama VAT (Kwa kila manunuzi yanayolipiwa VAT); PAYE; income tax, withholding tax, nk. Hii haijalishi kama ni taasisi ya serikali au la maana wao pia wanalipia VAT.

Ni vema katika reasoning yetu tukatambua kuwa katika bajeti ya serikali ya matrilion, kuna manunuzi makubwa yanayofanyika ambayo yanalipiwa VAT na pia kuna kodi za namna nyingine. Hii haijalishi kama taasisi hizi zinahusisha pesa za ruzuku za serikali au ni mapato yao wenyewe.

@Pasco listi hii ni ya mwisho wa mwaka wa serikali: End of June 2013. Nitakuja na list ya private companies.
 


Khaaa mbona sielewi. Mi nadhani kuna mataasisi mengi hapo yangekuwa kategorised kama . WATUMIAJI WAKUBWA WA KODI .
 

Hii orodha imeitwa ya walipa kodi wakubwa. Nikiri kuwa vigezo vyake sivifahamu. List ya private sector nitaitoa baadaye.

Haaaa haaa hiyo ya Krish ngoja nii google . . . thanks though!
 

Hello Pasco mashirika mengi uliyoyaorodhesha ni wakusanyaji kodi nna ada kubwa. Issue hapa ni kulipa kodi. Mfano TCRA wanakusanya royalty kubwa toka makampuni ya mawasiliano kwa niaba ya serikali lakini haina maana wao wanalipa kodi kubwa pia as TCRA.

List ni ya June 2013.
 
Last edited by a moderator:
Hapa naona list ya wala kodi ... (mashirika yaoishi kwa kutegemea kodi)

Hilo nakubaliana nalo mfano wizara za serikali. lakini wanapfanya manunuzi pia wanalipa kodi nk.
 
Breweries ndiyo wanaongoza kwa kulipa kodi Tanzania.

Ni kweli kabisa: Source: Home



Hata hivyo list yangu ni ya taasisi za umma na serikali. Nitatoa baadaye ya taasisi binafsi.
 
DAWASA ipo na ndio inamiliki miundo mbinu mikubwa ya maji, DAWASCO ni operation company na wachuuzi wa maji!

Pia inawezekana wana manunuzi makubwa kwa ajili ya hiyo miundombinu na hivyo kulipia VAT?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…