Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Umeruka swali alafu ukiwa kitu hujui au hukifahamu ni vizuri useme haujui kuliko kuruka swali unajipunguzia credibility yako ya maana, nimekuuliza unamjua msanii wa kwanza wa bongo alieachia ngoma radioni alikua anaitwa Nani? Kipindi hicho walikua wanabadirisha nyimbo za kingereza kuimba kiswahili yaan ngoma ya mbele Ila wanatafasiri mistari na kuimba kiswahili unamjua?
Hebu mtu mmoja aniwekee song la ice ice baby la saleh jabir. Nina swali hapa, hivi saleh jabir wa ruka kama ninja tua kama ndege ndio huyu presenter wa efm radio leo? Na je ana undugu na salama jabir?

Nilikuwa mdogo kipindi saleh jabir anaintroduce swahili rap na ngoma yake ya ice ice baby.
 
Kalapina,

Huyu jamaa mbali na kuwa na harakati nyingi akiwa pamoja na kundi lake la Kikosi cha mizinga .ukweli ni kwamba hana kipaji cha music. Alipata umaarufu coz ametoka kipindi wasanii ni wachache

Sugu

Huyu jamaa ana majina kibao kama Mr two, jongwe, too proud na sasa anajiita Taita licha ya kuwa na heshima kama moja ya waasisi wa music wa hiphop tanzania , ukweli ni kwamba hana kipaji cha music

Jaffarai

Huyu ni moja ya member wa wateule alitamba na wimbo wa niko bize .lakini hakuweza kudumu kwenye game kwa muda mrefu kutokana ukweli hana kipaji

Mchizi mox

Huyu pia ni member mwingine wa wateule ngoma zake zilizowahi kupata airtime ni mambo vp na chupa nyingine . lakini uwezo wake ni wa kawaida sana

Mike tee mnyalu

Huyu jamaa alipata airtime miaka ya zamani kwa ngoma zake lakini ukimskiliza ni wazi hana uwezo kabisa. Ni moja kati ya wasanii ambao huwa wanaandikiwa

Soggydog hunter

Huyu jamaa bora angebaki kwenye u presenter tuu huku kwenye music aliforce tuu hana uwezo kabisa ana ngoma nyingi ila iliyopenya ni kibanda cha simu pekee yake

Bou nako

Huyu alikua member wa N2N lakini tangu hakua na uwezo kabisa .nafkir wana walimbeba tuu kutokana na love .ila kwenye music jamaa hana kipaji

Kr mulah

Huyu ndio founder wa style ya kucheza Mapanga . ameanza sanaa muda mrefu sana lakini ukimskiliza utagundua jamaa hana uwezo wowote kwenye music kwa kifupi hana kipaji

Mh temba

Huyu ni member wa TMK wanaume family mwanzoni alibahatisha ngoma kama tatu zikaenda mjini, baadaye akaja kuungana na chege wakatoa hadi album..ila ukimfuatilia vizur jamaa hana
uwezo kabisa

Rich one

Huyu pia ni member wa TMK alitamba na ngoma moja aliyomshirikisha Juma nature inaitwa hatuna kitu.baada ya hapo hajawai kutoa hitsong tena, Jamaa anasifika kwa utapeli wa kuandaa show na wasanii fake huko mkoani afu anapiga hela

Dudu baya

Huyu jamaa aliotea ngoma kama tatu tuu ambazo zilimtambulisha vyema kwenye game .lakini alipata jina kwakua kipindi anatoka hapakua na upinzani mkali kama ilivyo sasa

Maujanja suppliers

Hawa jamaa nawakubali kwa harakati zao za street lakini kwenye music watupishe hawana vipaji .lakini wao wamekua wanalalamika wanabaniwa kitu ambacho sio ukweli

Kama unafuatilia music wa bongo fleva utakua unakubaliana na mimi hawa jamaa hawana talent za music kabisa

Kalapina (YES)
Dudu Baya (YES)
Richie One (YES)
KR Mullah (YES)
Bou Nako (YES)
Maujanja (YES)

Mchizi Mox (Muombe Msamaha)
Jaffarai (Muombe Msamaha)
Mh. Temba (Muombe Msamaha)
Sugu (Muombe Msamaha)

Mike Tee (Nenda palee upigwe makonzi manne, kisha muombe msamaha)
Soggy Doggy (Nenda paleee upigwe makonzi 9, kisha umuombe msamaha)
 
Hebu mtu mmoja aniwekee song la ice ice baby la saleh jabir. Nina swali hapa, hivi saleh jabir wa ruka kama ninja tua kama ndege ndio huyu presenter wa efm radio leo? Na je ana undugu na salama jabir?

Nilikuwa mdogo kipindi saleh jabir anaintroduce swahili rap na ngoma yake ya ice ice baby.
Kipindi hicho na wewe ulikuepo mkuu?
 
Unataka aweje ili umuone ana kipaji
Nikusaidie kwa mazingira ya zaman ilikua ni ngumu sana kutoa nyimbo na ukavuma ni tofauti na sasa hivi

Chujio la zaman ni gumu sana kama huna kipaji tofauti na sasa hivi mafanikio ya msanii yako revolve around kick
Hao uliowataja ni wachache kati ya wengi waliopambana kujulikana ki-music na wakashindwa ukweli ni kwamba watoto wa sahivi mnachukulia mambo kirahis sana kabisa unasimama unasema sugu au temba hana kipaji hivi unayajua mazingira ya 2000 kurudi nyuma huko
Ebu nikuulize una miaka mingapi
Mkuu haijalishi mtu ame hustle muda gani kutoka kimuziki , mimi hapa naongelea pure talent ndo nakwambia kwa wenye sikio la music MH temba hana kipaji
 
Kuna wasanii hapo siwakubali kwa personal interest ila siwezi kusema hawana vipaji.

Mtu kama KR ni vile tu jamaa kama hana bahati, ila mtu ambaye ana flava zake nzuri tu.

Enzi za 1. Kipe kitu 2. Mzee mwenye nyumba 3. Mguu nje mguu ndani n.k. waaay back akiwa GWM.
 
Mike T,Sugu,Jafarai, umefeli pakubwa.

Wasanaii wa siku hizi ndio bure kabisa zamani kupenya redioni mpaka kwenye kaseti sio mchezo kwa Dudubaya ni sawa jamaa hana upeo kabisa wa mziki.
Hao wote uliowataja waambie watoe hit song kwa kipindi hiki kudhihirisha ukali wao ..hao wote hawana uwezo
 
Huyo ni mtoto wa juzi anafikiri mazingira ya wakati ya miaka 90's ni sawa na leo ni tatizo kubwa la vijana wa social media ndo maana nikaamuliza kazaliwa lini isije ikawa unabishana na mtu ambaye kazaliwa 2000's ndo maana anaongea pumba
Nimezaliwa 1994/, nimeanza kuskiliza bongo fleva 1999 so nna experience kubwa sana
 
Back
Top Bottom