Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Kalapina,

Huyu jamaa mbali na kuwa na harakati nyingi akiwa pamoja na kundi lake la Kikosi cha mizinga .ukweli ni kwamba hana kipaji cha music. Alipata umaarufu coz ametoka kipindi wasanii ni wachache

Sugu

Huyu jamaa ana majina kibao kama Mr two, jongwe, too proud na sasa anajiita Taita licha ya kuwa na heshima kama moja ya waasisi wa music wa hiphop tanzania , ukweli ni kwamba hana kipaji cha music

Jaffarai

Huyu ni moja ya member wa wateule alitamba na wimbo wa niko bize .lakini hakuweza kudumu kwenye game kwa muda mrefu kutokana ukweli hana kipaji

Mchizi mox

Huyu pia ni member mwingine wa wateule ngoma zake zilizowahi kupata airtime ni mambo vp na chupa nyingine . lakini uwezo wake ni wa kawaida sana

Mike tee mnyalu

Huyu jamaa alipata airtime miaka ya zamani kwa ngoma zake lakini ukimskiliza ni wazi hana uwezo kabisa. Ni moja kati ya wasanii ambao huwa wanaandikiwa

Soggydog hunter

Huyu jamaa bora angebaki kwenye u presenter tuu huku kwenye music aliforce tuu hana uwezo kabisa ana ngoma nyingi ila iliyopenya ni kibanda cha simu pekee yake

Bou nako

Huyu alikua member wa N2N lakini tangu hakua na uwezo kabisa .nafkir wana walimbeba tuu kutokana na love .ila kwenye music jamaa hana kipaji

Kr mulah

Huyu ndio founder wa style ya kucheza Mapanga . ameanza sanaa muda mrefu sana lakini ukimskiliza utagundua jamaa hana uwezo wowote kwenye music kwa kifupi hana kipaji

Mh temba

Huyu ni member wa TMK wanaume family mwanzoni alibahatisha ngoma kama tatu zikaenda mjini, baadaye akaja kuungana na chege wakatoa hadi album..ila ukimfuatilia vizur jamaa hana
uwezo kabisa

Rich one

Huyu pia ni member wa TMK alitamba na ngoma moja aliyomshirikisha Juma nature inaitwa hatuna kitu.baada ya hapo hajawai kutoa hitsong tena, Jamaa anasifika kwa utapeli wa kuandaa show na wasanii fake huko mkoani afu anapiga hela

Dudu baya

Huyu jamaa aliotea ngoma kama tatu tuu ambazo zilimtambulisha vyema kwenye game .lakini alipata jina kwakua kipindi anatoka hapakua na upinzani mkali kama ilivyo sasa

Maujanja suppliers

Hawa jamaa nawakubali kwa harakati zao za street lakini kwenye music watupishe hawana vipaji .lakini wao wamekua wanalalamika wanabaniwa kitu ambacho sio ukweli

Kama unafuatilia music wa bongo fleva utakua unakubaliana na mimi hawa jamaa hawana talent za music kabisa
Wewe ni nani?
 
Unanikosea heshima
 
Nakumbuka nilisikiliza interview moja wakati huo pale radio one, UVC wakachana sana wimbo wa niko busy ( sikumbuki kama mashairi yalikuwa yale yale 100% au la). Na nika appreciate wimbo ni mkali so nasubiri utoke sasa.


Baada ya muda naona unatoka ila kaimba Jafarhymes, nkajua tu hapa biashara imefanyika.
Dah hiki kitu sikawahi kukijua
 
Ngoja tumnyonyoe liverfool then ntakuja hapa

Temba
Kiulaini
Nipe Mimi
Nampenda yeye
Mwaka wa shetani
Nawafunza kwa maneno
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Hizo ngoma zote ni before 2010

Niambiea kuanzia 2011 kutoa hit song gan kama solo project
 
Back
Top Bottom