Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Ipo Swaken kinyerezi na nyingine Mbweni chumba kimoja na sebule! Downtown ni kwenda kupiga picha kwenye appartment za watu i'm humbled you know!
Boma Ye hivi kweli ana nyumba Mbweni?
Eheee amejenga Hidden servant kota ,chumba kimoja na sebule.
basi amejitahidi maana kwa bata zile anazokula! nishaona akielezea ana mjengo Mbweni nikajua ni fix tu kwasababu yule ni mtu wa 'kamba kamba' yule. unajua hata kiwanja cha Kinyerezi wanasema alipewa na wakwe ndio maana inakuwa tabu kuhamia.
 
Kenge wa Mahenge wewe !! Kila mtu akijenga nani atapanga ?!
 
Ila unaishi kwenye nyumba walizojenga wenzio? Kama nyumba siyo mhimu, si uishi porini? Duniani si unapita tu?
Hawa ndiyo wanaosema gari sio muhimu lakini kutwa utawakuta barabarani wanasubiri lifti za wenye magari binafsi wagongee au anaamka saa 11 ili awahi daladala ,sasa kama gari siyo muhimu si watembee kwa miguu.
au kama nyumba siyo muhimu si wakaishi Porini kama wanyama wasipange kwenye nyumba za watu wengine.
 
Hapo chacha
 
Hapo chacha

Huwa wanazingua sana na wanaboa kinoma! Hawataki kukubali kwamba hawana hela ya kununua gari au kujenga ila wanajificha kwenye gari siyo muhimu as if anatembea kwa mguuu akienda kwenye shughuli/kazini kwake au analala nje barabarani au porini kama nyumba siyo muhimu.

Hakuna mtu anayetaka shida hata mmoja sema ndiyo hivyo tu usawa unakaba ,haya mambo ya kusema sijui Elon musk hana nyumba ni udwanzi tu ,sasa kama mtu amenunua Twitter na baadhi ya mali zake zote including baadhi ya majengo yake napo utasema hana nyumba? Wanataka kusema biashara zake zote anazifanyia kwenye majengo ya kupanga?
 
No.6😅😅😅😅😅😅😅😅😅
 
Ahaaa umeongea point mkuu
 
Ila kujenga kuna faida zaidi ya kutojenga, nashindwa kuelewa kwa nn wanachagua kutojenga.

Kuna msemo waswahili wanasema "bora ulale njaa kwako"
Humu siku hizi watoto ni wengi sana wasikusumbue akili pia watu wenye stress.

Mada hii ingeletwa hapa 2013/16 comments za kitoto toto usingeziona humu,hakuna mwanaume kamili anayetafuta hela na ana familia aseme kwa sababu duniani tunapita basi hakuna haja ya kujenga,waulize baba zao hawakujenga?wao wamekulia wapi,porini?
 
Akili kubwa za kuutafuta utajiri pasipo kujali wengineo. Siyo mbaya kutafuta, tatizo ni pale unapotumia nguvu kubwa na kuathiri wengi wakati utaviacha na hujui utakao waachia watavitumiaje
 
Siyo lazima kila mtu ajenge nyumba. Wengine watabaki wapangaji maisha yao yote
Hivi miji kama Tokyo, new York watu wanawaza kujenga kweli?
Mifumo ya maisha ya hao watu wa huko ni tofauti sana na sisi wa huku. Wao wanawaza kujiendeleza kielimu zaidi wakati sisi tunatazama future kwa namna tofauti na wao. Sisi tuna fursa ya kujenga kirahisi zaidi kuliko wao. Na mambo mengine kama hayo
 
Imagine[emoji848]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…