Orodha ya watanzania wanaofaa kushika nafasi ya ukurugenzi TPDC

Orodha ya watanzania wanaofaa kushika nafasi ya ukurugenzi TPDC

Nakuomba upitie CV ya mzee Mataragio kwanza kabla hujaendelea na comments nyingine
achana na mambo ya CV, huu uzi lengo lake ni kwaajili ya future kama hawa wakina mataragio hawatakuwepo.
 
Kuwa Ulaya is one thing.
Haya mambo ya kitaalam yana specialization pia.
JK did very well wakati wake to bring back vichwa ktk sector mbalimbali, na akawapa packages nzuri sana !
Akaja mshamba mmoja, akavuruga kila kitu !
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dkt. James P. MATARAGIO kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).


Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.

Dkt. James P. MATARAGIO ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani. Wasifu wake ni kama ifuatavyo:-


ELIMU:-

· Masters in Business Development (MBA), Chuo Kikuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)

· PhD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)

· MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)

· BSc(Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994


UZOEFU WA KAZI:-


· Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA

· 2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu

· 2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

· 1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)

· 1994 – 1999 -, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.


Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.


Aidha, Dkt. James P. MATARAGIO ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia waishio Marekani (Diaspora) ambao walijitolea kuishauri Serikali kuhusu sekta hiyo bila malipo.


Kwa kuzingatia elimu yake, uzoefu wake na uzalendo wake, Rais ana matumiani makubwa kuwa Dkt. James P. MATARAGIO ataleta nguvu mpya na uzoefu mkubwa wa kimataifa katika kuiongoza TPDC ili iwe kampuni kubwa ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia kama yalivyo makampuni mengine ya kitaifa ya mafuta na gesi asilia duniani.
 
Haya mashirika makubwa huwa kigezo cha kwanza wanaangalia ni mtiifu kwa ccm?
ccm wanapotaka kuiba au wanapotaka hela kwa ajili ya mambo yao hela inatoka huko.
 
Sasa mataragio mfano akafa nani atakaye mrithi mkuu? hili ndio lengo la huu uzi. Na ndio sababu nakusisitiza upendekeze jina lingine
Huo ni uchuro ni sawa na kusema tuanze kutafita jina la nani awe raisi badala ya aliyepo
 
Haya mashirika makubwa huwa kigezo cha kwanza wanaangalia ni mtiifu kwa ccm
Ndio lazima aikubali CCM na sera yake kuhusu bandari ulitaka awe mtiifu mfano kwa Chadema wataka kuuza mali za umma kupitia MIGA?
 
Zingekuwa teuzi ndio zinafanywa hivyo hata sisi wa Buza tungepigiwa simu tukawe wakurugenzi wa hiyo TPDC,hauwezi kuteuliwa kama haupo kwenye system na kwenye cycle yao.Lazima huwe mtu wa kitengo kwanza.
 
Hujatoa option ya watu kujitaja wenyewe. Ungekuwa umefanya hivyo ningeweza kujitaja....lol
 
Huyo no.2 mbona ni mtaalamu wa IT
IT na TPDC wapi na wapi?.

CV ya Mataragio bado iko imara sana
Na Mungu ana nia nae kila wakimtoa anarudi..twice now!
 
Back
Top Bottom