Orodha yangu ya waandishi wa vitabu na watunzi wa stori..

Orodha yangu ya waandishi wa vitabu na watunzi wa stori..

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Hi..
Kama wewe ni mpenzi wa kusoma vitabu au stori mbalimbali itakua kuna watunzi utakua unawakubali, kuna watu wamejaliwa vipaji sana humu duniani yaani ukisoma kitu unajiuliza alifanyaje hadi akatunga kitu kama hiki. Unakuta stori imepangwa ikapangika akili kubwa imetumika. Binafsi hii ndio orodha ya watunzi na waandishi wa stori ninao wakubali zaidi katika historia yangu ya kusoma soma vitu (Fasihi andishi)
  • Paulo the Apostle
Huyu jamaa alikua ni mkazi wa Tarso alikua ni mfuasi wa Yule bwana mdogo mashuhuli niliyemzungumzia siku chache zilizopita, kaandika vnyaraka nyingi sana zenye kuelimisha na kuonya. Anahesabika kama moja ya mwanafalsafa mkubwa aliyeishi hapa duniani. Kazi zake zimesomwa na zinaendelea kusomwa na watu wengi kila siku. Maandiko yake yanaitwa Pauline epistles au nyaraka za Paulo ambazo baadhi ni waraka kwa waroma,waraka kwa wakorinto 1,2,3&4,wagalatia,waefeso,timotheo,tito,waebrania nk. Huyu jamaa kafanya makubwa sana kutokana na uandishi, kachangia sehemu kubwa ukristo kuwa kama ulivyo. Wengine huenda mbali zaidi na kusema kua alishirikiana na warumi kutengeneza ukatoliki.
  • Luke the Evangelist
Mbali ya kua mwandishi pia alikua ni mchoraji na kwa upande wa kitaaluma huyu mtu alikua ni Daktari alikua ni mkazi wa huko antokio. Kaandika stori safi sana ya kijana Yesu.Aliandika kwa ufanisi mkubwa pia anakumbukwa kwa kuandika kitabu cha matendo ya mitme. Akielezea mambo mbalimbali waliyotenda wafuasi wa Yesu. Tunamkumbuka kwa uandishi wa injili yake safi inayofahamika kama Injili ya Luka.
  • Stan Lee
Kwa jina la kuzaliwa anaitwa satnley Martin Lieber kazaliwa December 28 1922 kafariki mwaka 2018 November 12 akiwa na miaka 95. Huyu jamaa alikuwa mwandishi na mtunzi wa comics (story za superheroes) katunga comics nyingi sana alikuwa anafanyia kazi kituo cha uandishi wa comics kiitwacho Marvel Comics, karibia asilimia 60% ya comics zote za America kuna mchango wake. Katunga superheroes maarufu kama vile Iron Man,Captain America, X-Men,Spiderman,Hulk,Captain Marvel,Thor,Doctor Strange,Blade,Ghost Rider,Black Panther na nyingine nyiiiingi sana. Binafsi huyu kwangu ndio muandishi namba moja kwangu, yaani hua nafikiria hizi stori alikua anazitoa wapi na inaonekana alikua mtu genius sana .

Comics za Iron man zimetungwa miaka ya 1950 teknolojia ya Artificial Intelligence haijawa official known lakini jamaa alitunga kama vile ni stori za miaka ya sasa teknolojia ikiwa kubwa. Japo kwenye mythology wanatambua kulikua kuna mungu anaitwa thor ila jamaa stori ya thor sijui aliiweka vipi yaani. Kiufupi jamaa alikua genius sana sioni Mwingine zaidi yake kama nikiwatoa Luka na Paulo.
  • Paul T. Scheuring
Huyu jamaa anaweza kua sio maarufu sana ila jamaa ni bonge moja la mtunzi, sijui ana akili ya namna gani huyu mtu maana kwa visa alivyotunga itakua ni mtu mwenye IQ kubwa sana. Katunga stori ambazo zilitengenezewa muvi naseries maarufu zaidi duniani. Alitunga kisa cha Prison Break na Muvi ya Den of Thieves iliyotoka mwaka 2018 na nyingine nyingi ambazo kama ukiziona utakubaliana name huyu mtu anajua kuutumikisha ubongo katika kufikiria.Binafsi baada ya Stan lee anafuta huyu, naamini hawa watu wana akili sana.
  • Raymond Marshall
Hili jina sio maarufu kwa wengi, lakini huyu ni moja kati ya waandishi mashuhuli waliopata kuishi hapa duniani katika uandishi wa novel za kijasusi. Anafahamika zaidi kwa jina la James Hadley Chase. Wanamwita kua ndio king wa utunzi wa novel za kijasusi kwa visa vyake vyenye utata. Kaandika novel nyingi sana kama 50+ siwezi kukwambia kua kasome hii au hii, wewe tafuta kitabu chake chochote soma lazima ukipende tu maana vyote ni vizuri sana. I wish ningekua nina uwezo kama wa huyu mtu.
  • William Shakespare
Huyu baharia yeye aliishi karne ya 16 huko, ila katunga novel na Mashairi mengi sana..wanasema hakua na elimu kubwa ila alikua anaandika vitu ambavyo kwa mtu kama yeye hawakuelewa alikua anavitoa wapi. Wengine wanasema alikua anatumika na watu ili kuandika vitu anavyoambiwa aandike. Ila ukweli utabaki pale pale kua alikua mtu smart sana. He is my role model.

Wa mwisho naomba nimuweke Rick Warren kaandika kitabu cha Purpose driven to life. Alijitahidi sana. Ni hicho tu na penda toka kwake na pia Dan Brown alijitahidi sana na Novel zake.

Je wewe waandishi wapi unawakubali zaidi?
 
Binafsi nitakua sijatenda haki kama sitawaweka hawa writters by David Benioff na D. B. Weiss.
Hawa majamaa naweza sema ni watu smart sana kuliko..katika uandishi wa matukio/scripts na kuandika dayolojia.
Hawa ndio wametengeneza Series ya Game of thrones, kwa jinsi walivyoipangilia matukio,maongezi na kila kitu...naweza sema hakuna mwingine mwenyw uwezo kama hawa jama.
Kingereza kimetulia cha zamani.
Ukitaka ujue hawa jamaa wanajua kupangilia maneno na misemo fuatilia mazungumzo ya Tyrion Lannisters (The Dwarf/Imp) utakubaliana nami...Usipokua makini huwezi kuelewa
 
Writters wengine naowakubali kazi zao zaidi ni..
Christopher Markus na Stephen McFeely, hawa jamaa nimewakubali kazi zao. Wanajua kupangilia stori na kuumda maongezi yenyekuvuti. Wameandika dialogues za Avangers endgame,Captain America winter soldiers and Civil war, Thor,infinity war,nk nk




Paula Paul
 
Ifike wakati muwape nafasi hata waandishi wazalendo sio kila siku wa huko mbele tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hapa tanzania nawakubali waandishi hawa..
  1. Ben Mtobwa (nimesoma karibu vitabu vyote)
  2. Kevin Mponda (simulizi zake zipo humu)
  3. The Bold (Mwana Jf)
  4. Mwandishi wa simulizi za Will Gamba
 
Shaban robert....kitabu na page 70 wiki ya pili sijamaliza. #kusadikika mwandishi #48lawsofpower. ? Dah...wengi mzee waandika biblia na quran
 
nimepata kusikia na baadae nikasoma online kuwa Shakespeare did not really exist yaani hakujawahi kuwa na mtu aliyeitwa Shakespeare isipokuwa ni masimulizi tu kama habari ya wahenga kibongo bongo ambao kwa hakika hawajapata kuwepo ila ni msemo tu au sawa na Confucius kwa wachina he never existed ila ukifuatilia utaonyeshwa mpaka kaburi lake but kwa uhalisia hajawi kuwepo huyo Confucius. hatari sana
 
nimepata kusikia na baadae nikasoma online kuwa Shakespeare did not really exist yaani hakujawahi kuwa na mtu aliyeitwa Shakespeare isipokuwa ni masimulizi tu kama habari ya wahenga kibongo bongo ambao kwa hakika hawajapata kuwepo ila ni msemo tu au sawa na Confucius kwa wachina he never existed ila ukifuatilia utaonyeshwa mpaka kaburi lake but kwa uhalisia hajawi kuwepo huyo Confucius. hatari sana
Kuhusu shakespear kuna Nadharia nyingi sana. Kuna conspiracy theory moja inasema kua Williams stories zake zote alikua anaandikiwa na mama mmoja mtumwa mweusi. So willy hakutunga lolote aliweka jina lake tu..
 
Kuhusu shakespear kuna Nadharia nyingi sana. Kuna conspiracy theory moja inasema kua Williams stories zake zote alikua anaandikiwa na mama mmoja mtumwa mweusi. So willy hakutunga lolote aliweka jina lake tu..
Inawezekana kabisa, Ila zote zitabaki kuwa conspiracy theories
 
Ila kumuelewa Stephen Hawking lazima na wewe uwe msomi tena wa kiwango cha hesabu na fizikia. Nimesoma kile
" a brief history of time"
Stephen hua nadhani ni Clone ya Einstein. Hawa majamaa kuwaelewa isue
 
RIP STAN LEE
FB_IMG_15789508883054554.jpg
 
Back
Top Bottom