Oscar Oscar, kama kumuita kiongozi wako mpuuzi sio kosa, fanya hivyo basi kwa bosi wako Majizo kama utabaki salama

Mpuuzi maana yake ni mtu anayepuuzia kitu sio tusi, Haji aanzie BAKITA then akate rufaa anashinda mapema tu.
Hana ubavu wa kukata rufaa, si mlimsikia aliomba msamaha kabisa kabla ya kupigwa ban, Haji anajua alikosea kumkoromea rais wa tiefuefu hilo ban ni haki yake ashike adabu
 
1. Aliomba msamaha nje ya TFF na si ndani ya TFF

2. Amekiri kosa kwa kutia doa tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu,

3. Alitishia maisha ya kiongozi wa TFF hilo ni kosa la jinai. Adhabu ni haki yake.
 
Ninaposoma comments za wadau hapa ndo nagundua watanzania wengi bado ni wajinga sana!
 
Kinachosikitisha ni kwamba hawa ndio think tank wa soka letu, so sad.

Kuna watu wanaojiita wachambuzi Kuna mambo wanayazungumza nyuma ya mic 🎤 unabakia kujiuliza huyu ana utimamu wa akili Kweli?
shida ni media zetu zimewapa jukwaa watu wajinga wajinga tu. iwe kwenye soka au siasa
 
Wewe nawe mtoto wa juzi bila Manara ungeipenda makolo? Hao TFF ktk ushahidi wao hakuna sehem waliposema Manara alimuita Karai the Bogus Mpuuzi... Usikurupuke kijana, hii ni michezo halafu mwisho wa siku ujue watoto wa mjini ndio watakao maliza huu mzozo kwasababu karai na ukubwa wake wote hana chochote anachojua pale TFF
 
Kwahyo Manara boss wake ni Karia tumbo tumbo?
 
Anayemtetea manara nae ni mpuuzi pia...

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Kwahyo Manara boss wake ni Karia tumbo tumbo?
Maadamu anaweza kumwadhibu basi kwa namna fulani anaweza kuwa bosi wake. Ni tofauti na mimi ambaye hata nikimtukana vipi huyo Karia hana la kunifanya zaidi ya mahakama.
 
Kinapokuja swala la kutetea maswala yanayohisisha team mashabiki huwa mnaweuka kabisa.
 
Hivi huyu Oscar Oscar nae ni mwandishi mnamskilizaga kabisa. Mi naonaga tu tweet zake. Ni za kipimbi. Muhandishi muda wote ni tweet za ajabu ajabu tu
 
miaka ya hivi karibuni tasnia nzima ya mpira wa miguu hapa tz, imezungukwa na machawa kila kona.

machawa hatari zaidi ktk football ya tz ni waandishi wa habari za michezo, wanaojiita wachambuzi(field ya watu wajanja-wajanja) na watangazaji wa tv/radio wanaosimamia program za sports.

ukichunguza sana, unaweza kuta huyo oscar oscar yupo katika payroll ya gharib wa gsm. sio ajabu mtu kama huyo kujifanya mtetezi wa ujinga anaoufanya manara.

manara ni mtu wa karibu zaidi wa gsm, kwa hiyo usishangae chawa oscar oscar kujitoa akili kumtetea manara ilmradi tu manara alinde maslahi yake kwa gsm. njaa mbaya sana
 
Kinapokuja swala la kutetea maswala yanayohisisha team mashabiki huwa mnaweuka kabisa.
Kuna mahali nimetetea timu yangu! Mimi siku zote napenda haki. Malumbano yaliyojitokeza siku ya mechi ya fainali yalikuwa ni ya watu wawili! Sasa inakuwaje aadhibiwe mmoja?

Au mnataka kutuaminisha Wallace Karia ni mtu special sana kiasi hawezi kukosolewa! Halafu hiyo milioni 20 anatozwa faini kwa ajili ya nini! Na inaenda kwenye mfuko gani! Kama siyo wizi na uonevu.

Narudia tena kusema; sijawahi kumuunga mkono Haji Manara kwa sababu ya kejeli zake! Lakini linapokuja suala la haki, nitasimama kwenye haki.
 
Je kilichotukanwa, dhalilishwa, tusiwa ni cheo cha Urais wa TFF au mtu anayeitwa Karia?

Isijekuwa Manara na Karia wana 'bifu' zao binafsi, hivyo mwenye kulalamika angepeleka malalamiko yake kwenye vyombo vya kisheria vya nchi...

Karia angelifanya kama Membe alivyofanya kwa Musiba, Membe hakutaka Musiba aadhibiwe na chama bali mamlaka za kisheria za nchi ili iwe funzo kwa wengine, na kuziba mwanya wowote wa Musiba kuendelea kukashifu Membe
 
Akili Hana ndo Mana alishindwa urais tff
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…