Oscar Oscar, kama kumuita kiongozi wako mpuuzi sio kosa, fanya hivyo basi kwa bosi wako Majizo kama utabaki salama

1. Aliomba msamaha nje ya TFF na si ndani ya TFF

2. Amekiri kosa kwa kutia doa tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu,

3. Alitishia maisha ya kiongozi wa TFF hilo ni kosa la jinai. Adhabu ni haki yake.
Aliomba msamaha and still akapeleka mawakili

Aliprleka mawakili wakazi gani na wakati alikwisha ungama kuwa alikosea?

Na mawakili ndio waliokuja kumchomesha, wiki iliyopita nilimsikia wakili wake akihojiwa kwenye kipindi cha Sports HQ

Wakili alisema kwa mujibu wa sheria kosa alilotenda manara halijaoridheshwa katika list ha makosa

Na sheria inasema mtu anayejaribu kutoa hukumu kwenye kosa ambalo halijaainishwa na sheria basi kibao kinamgeukia yeye

Maulid kitenge akamuuliza kwa hiyo una maanisha nini? Wakili akasema kesi imewageukia wao yani wao ndio wana kesi ya kujibu

Ukiwa na mawakili wa namna hiyo ni mzigo sana yani hata kesi ya kukanyaga nyanya sokoni unaweza fungwa maisha
 
Hastahili adhabu au HASTAHILI ADHABU ILE?
 
Ninaposoma comments za wadau hapa ndo nagundua watanzania wengi bado ni wajinga sana!
Soma na hii nami uniongeze kwenye list

Huwa sipendi kubaguliwa kizembe
 
Aliomba msamaha wa nini?

Halafu kwanini atume mawakili kwenda kumtetea kwa dhana ya kwamba hajafanya kosa?

Ikikuuma mchangie 20M

Byuti byuti
 
Rasta

Yule alikuwa ni haji anatoa maneno machafu na kumtishia Karia kuwa hamuogopi

Karia alikuwa akimuonya kwa kumnyooshea kidole na hata mashahidi waliokuwepo wamekiri.
 
Poleeeeeeeh. Kamsaidie kulipa faini shogaaa ako Takadini.

Byuti byuti
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama 95% ya Bia za Bure anazokunywa Oscar Oscar na 'Migoma' yake anayoikota hovyo huku Mmoja akiwa ni wa Mji Mpya Kawe ameshaungua kwa Moto ( Waya ) ni kutokana na Msaada na Umaarufu wa Swahiba wake Mfungwa Mpya Michezoni Haji Manara unategemea / ulitegemea nini Mkuu?
 
Mpuuzi maana yake ni mtu anayepuuzia kitu sio tusi, Haji aanzie BAKITA then akate rufaa anashinda mapema tu.
Sawa ..mtoa Uzi hana shida na hilo..amesema huyo Oscar akamuambie hivyo boss wake Majizo kwamba ni mtu anayepuuzia mambo aone
 
Huyu karia alivyowakata wale wagombea wengine wa urais TFF nilimuweka kundi moja na Akina manara na Oscar Oscar
 
Haji Manara amekiri mwenyewe kuwa alimkosea Karia hadi akaenda kuomba radhi sasa wewe ni nani kupingana na nafsi ya Haji Manara? Kumbuka Haji ana makosa ya kujirudia rudia. Pamoja na yote amepewa nafasi ya kukata rufaa
 
Hivi una habari aliyefungua shauri ni secretariat ya TFF na siyo Karia? Haya ni mambo ya michezo na yanashughulikiwa kwenye vyombo husika.
 
Mkuu naomba nikuulize kitu mfano lile ni jukwaa kuu AKA VIP Basi kwa maana hyo hata kiongozi wa nchi angekuwepo siku hyo angeweza kukaa pale au maeneo Yale Yale Sasa swali la msingi manala angefanya huo upuuzi mbele mheshimiwa Raisi wa jamhuri je angeachwa salama kwa kisingizio kuwa alikuwa Na munkari???
 
Mpuuzi maana yake ni mtu anayepuuzia kitu sio tusi, Haji aanzie BAKITA then akate rufaa anashinda mapema tu.
Aliyesema kuwa 75%, ya watanzania ni walemavu wa akili hakukosea maana tayari mwingne huyu hapa
 
Bahati mbaya hiyo nafasi asingeipata. Maana kuna watu wa usalama wangeweza kutimiza majukumu yao kwa wakati.
 
Bahati mbaya hiyo nafasi asingeipata. Maana kuna watu wa usalama wangeweza kutimiza majukumu yao kwa wakati.
Sasa kwann asiiheshimu ile nafas? Na ndo amepigwa nyundo kisa hicho pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…