P Funky Majani (Godfather wa Bongofleva) ni mzaliwa wa wapi? Je, ni mtanzania halisi au kachanganya?


Yaani uishi na kina Kobe Bryant miaka 5 asubuhi upo nao jioni upo nao mchana upo nao..mazoezini kambini na kwenye mechi halafu eti ubaki tu kuongea kama kingwendu??..huo utakua sio tu ulofa ila utakua ufala..lazima ubebe swaga za mtoni..hao mnaowaona wanakaa mbele na wakirudi wanaongea kama senga ujue walikua wanajifungia tu vyumbani huko..
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Samahani mkuu edit hapo kwenye kundi LA cleptomaniax hiyo sentensi inayofuata imeharibu maana
 
 
Huyu kijana Hashimu Thabiti (Hasheem Thabeet) Kama anavyojiita siku hizi, ndio huwa ananishangaza sana mkuu. Maisha aliyotokea na muda alioishi States eti Kiswahili kinampa shida!!!!!! Huwa nachoka kabisa nikimsikia anaongea.
Ubishoo tu mkuu...wakati mimi nina miaka 17 nje ya eneo la nyumbani but lugha yangu haijawahi kunipiga chenga{sio kiswahili namaanisha lugha asili}huwa anajionaga vipi sijui na sio yeye tu wapo wengi sana hawa.
 
Huyo ni mchanganyiko nusu mtanzania vs mdachi[emoji12]
 
Haha [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] eti kama Senga...
 
Samahani mkuu edit hapo kwenye kundi LA cleptomaniax hiyo sentensi inayofuata imeharibu maana
Kaka usinge-quote post yake ungemu-alert tu kuirekebisha maana hata aki-edit kumbukumbu itabaki hapa ktk bandiko lako{nimekosa maneno ya kuweka huko nilikochanganya lugha}[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] .....
 
Hashim aliniacha Makongo form three,miaka ile ya 2004!
Alikuwa anarudiarudia masomo kwa kuzungusha mibashite!
Ila mpira wa kikapu ulimtoa!
Nakumbuka alivyokuwa anateseka kupanda vipanya vya Kawe Mwengea au Tegeta Posta kwa ule urefu wake!
 
Kaka usinge-quote post yake ungemu-alert tu kuirekebisha maana hata aki-edit kumbukumbu itabaki hapa ktk bandiko lako{nimekosa maneno ya kuweka huko nilikochanganya lugha}[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] .....
Sikugundua haraka mkuu imenitia ukakasi sio siri hizi simu mterezo ni kazi
 
Cha ajabu pamoja na umaarufu wote mpaka leo anaishi kwao na mama ake pamoja na familia yake
Cha ajabu ni kipi? Umaskini wako ndio umekufanya uishi mbali na wazazi wako.

Bakhresa mpaka leo anakaa na watoto wake wote pale Masaki.

Akili za kimaskini ni mbaya sana, nimefanyakazi KLM na mama yake Paul ni swahiba wangu mtoto ninayemjuwa mimi ni Paul na mama yupo mwenyewe hivi kuna ubaya gani mama kukaa na mtoto wake?

Chunguza kwa makini hata wahindi wanaishi kifamilia, hata huko mamtoni nimezunguka sehemu nyingi matajili kwenye Mansion zao wanaishi kifamilia.

Hizi dhiki zetu za kumaliza sabuni bafuni na kuongezeana gharama za chakula ndio zinasababisha kijana mdogo eti naye kapanga chumba!
Poverty.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…