Habari zenu ndugu zangu
Napenda kujua historia ya huyu producer mkongwe hapa nchini nimeangalia interview zake mbalimbali nimevutiwa na uwezo wake wa kuelezea vitu pia huyu jamaa ana content Sana hababaishi.
Napenda kujua asili yake kwa sababu kwenye interview zake nyingi anaonekana kiswahili kumpa shida sana katika uzungumzaji wake kama sio mbwembwe.
Ukifuatilia interview alofanya na dj Lil omy wa times FM utagundua nilichokisema
Hivyo basi nakaribisha michango yenu kwa anayejua historia ya P-funky majani
P. Funk
Paul Majani
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Paul Matthysse
Pia anajulikana kama P Funk, Majani, Kinywele Kimoja, Mdachi nk.
Asili yake Tanzania
Aina ya muziki Hip Hop na
Bongo Flava
Kazi yake Mtayarishaji
Ala Kinanda,Guitar, Kinakilishi
Miaka ya kazi mn.
1995 -
Studio Bongo Records
Ame/Wameshirikiana na Master Jay,
Bonny Luv,
Rajabu Marijani,
Bizz Man, Boznia nk.
Paul Matthysse (
P Funk ) ni
mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya
Bongo Records iliyopo jijini
Dar es Salaam,
Tanzania.
P Funk a.k.a. Majani, ambaye ni
nusu Mtanzania na nusu
Mdachi, kama miaka ishirini iliyopita alikuwa na hisia za kupendelea muziki na pindi hadi kuamua kufanya kweli kuvutiwa kwake kupenda muziki ndio chanzo kikubwa kilichopelekea kufanikiwa katika muziki.
Kwenye miaka
1991-
92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika. Alikuwa mtundu mtundu kwenye studio za pale shule.. kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga musiki kwenye Pati mbali mbali.. na hapo alikuwa kupenda sana musiki kwa ujumla.
Yaliyomo
[
1Elimu ya Muziki na Uzoefu Wake
Elimu ya Muziki na Uzoefu Wake[hariri | hariri chanzo]
P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale
Amsterdam,
Netherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya. Mwaka
1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya
Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa. Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo.
Anakubali kuwa amepata sana utaalam na mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.
Tuzo Alizopata[hariri | hariri chanzo]
Wasanii Aliowainua[hariri | hariri chanzo]
Kwanza alianza kwa kumpandisha chati
Juma Nature, ambaye ndio nyota wa nyimbo za
Bongo Flava, akaendelea kwa kutayarisha santuri ya
Solo Thang,
AY,
Zay B,
Sista P,
Mike T na pia alishawahi kufanya kazi na
Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe.
P Funk ana wasanii wengine wengi wanaotumia nembo ya kampuni yake katika utengenezaji wa albamu.
Pia Anajulikana Kama[hariri | hariri chanzo]
- P Funk
- Halfani
- Majani
- Kinywele Kimoja
- Mkono wa mungu

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni
mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu
P. Funk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari.
kazi ni kwako soma