Vijana wengi wa Kitanzania hususan hawa millennials hupata shida kuongea Kiswahili kitupu kilichonyooka.
We jaribu kumsikiliza yule mwigizaji Lulu uone.
Jaribu tu kuwasikiliza wabongo fleva...hata Diamond naye siku hizi kaanza kuwa hivyo.
Yule mcheza kikapu Hashimu Thabiti ndo kabisaaa....utadhani hajazaliwa Dar au Tanzania. Huwa anapata shida sana kuongea akiwa anaongea Kiswahili.
Sijajua hasa tatizo ni nini lakini ninahisi mojawapo ya sababu ni kutaka kujifanya u wa hali na hadhi fulani [kwa kuchomekea sana maneno ya Kiingereza] na pia kutokujua vizuri lugha yoyote ile, iwe Kiswahili au Kiingereza.