Nimeanza safari ya mpira toka nipo kinda, kipindi hicho Hata shule sijaanza, kipindi tunacheza mipira ya makaratasi barabara I au uwanja wa nyumbani (uwani), ni katika kipindi kicho ndo nikajizoeza kupiga miguu yote.
Nilipoanza shule nikaendelea kukiwasha, zile match za madarasa vs madarasa (let's say for example: std iii vs std iv )au mikondo vs mikondo (A vs B) nilikuwa nakiwasha balaa. Kumbuka hapo napiga peku peku.
Kuanzia darasa la 5 hadi darasa la 6 mimi ndo nikawa mlinzi namba 4 tegemeo wa shule. Kamwili kadogo,ila wepesi, speed, akili na passion vilinifanya nikawa beck ninaewadhibiti washambuliaji wakali. Tackling, acrobatics,kutibua mipango, vilinifanya kuwa maarufu sana
pale shuleni na kijiji kizima. Ni katika kipindi hicho 2005-2006+ ndiyo nilianza kufanya mazoezi na wakubwa kwenye timu ya kijiji.
Match ya kwanza kupangwa kwenye timu ya wakubwa ilikuwa 2006, nipo darasa la 6 hapo, nilipangwa beki 2, niliboronga sijui woga!!! Nikatolewa.
Kuanzia mwaka 2007 nikiwa darasa la 7, mimi na mwili wangu mdogo,ndiye niliekuwa full back tegemezi wa shule na kijiji.
Kuanzia 2008-2010(form 1-3) mimi ndiye niliekuwa mlinzi tegemezi wa darasa, wa shule (sekondari) na timu ya kijijini (walikuwa wananifata kila kukiwa na match.
Kuanzia mwaka 2010-2011 (form 3-4) mimi ndiye niliekuwa mlinzi tegemeo wa darasa, shule, timu ya kijiji na timu ya kijiji cha pale shule ilipokuwepo.
Nilianza kuacha mpira 2012 baada ya kwenda advance.
SAMAHANI MKUU KWA KUKUPA JIBU REFU SANA. NIMEJIKUTA NAWAZA MBAAAALI SANA!! ENZI ZANGU, KAMA HENOCK INONGA MTUPU!! ka mwili kadogoooo ila ninaowazuia watu wanabaki wanasema natumia madawa kumbeee chini ya kapetii......siri ya mchezo ni NILIKUWA NAFANYA MAZOEZI SANAAAAAAAAA