Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha imeeleza kuwa hali ya Neema ilibadilika ghafla akiwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU).
Aminiel Aligaesha amesema: "Nasikitika kukufahamisha kuwa mtoto Neema ambaye alitenganishwa na mwenzake Rehema amefariki jumapili ya tarehe 10 Julai saa 3 asubuhi. Akiwa ICU hali yake ilibadikika gafla, madaktari walijitahidi kurudisha hali yake bila mafanikio na hatimaye kupoteza maisha. Twendelee kumwombea Rehema ambaye bado yupo ICU ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema. Bwana alitoa na Bwana ametoa, jina lake lihimidiwe sana."