Maudhui ya kuogofya! Padri Patricio Alfredo Sánchez Molinari amefariki dunia nchini Ecuador baada ya msalaba mkubwa kuanguka na kumwangukia akiwa katikati ya ibada kanisani. Tukio hilo lilinaswa kupitia matangazo ya moja kwa moja (livestream).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kanisa Katoliki, Padre Patricio alikuwa akihudumu kama paroko wa Kanisa la Perpetuo Socorro, katika eneo la Vicaría Centro, jijini Guayaquil.
Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Guayaquil limetoa salamu za pole kwa familia yake, ndugu wa shirika la Redemptorist, pamoja na marafiki zake, huku likiwaalika waumini kuungana katika sala kwa ajili ya mapumziko ya milele ya roho yake.
Taarifa hiyo ya rambirambi ilitolewa Oktoba 17, 2026, na Kardinali Luis Cabrera Herrera, Askofu Mkuu wa Guayaquil.