Padre Dkt. Kitima: Aliyemuua Kibao tunamlaani, amefanya kosa baya, ni chukizo kwa Mungu

Padre Dkt. Kitima: Aliyemuua Kibao tunamlaani, amefanya kosa baya, ni chukizo kwa Mungu

Kama kanisa inafaa kuiombea Neema na Baraka za Mungu familia ya Mzee Kibao..

Lakin zaid sana kumuombea huruma ya Mungu muuaji wa Mzee Kibao.

Mengine nadhani sio wajibu wa kanisa bali inaweza kua uchochezi zaidi 🐒
Endeleeni kuua na sisi Kanisa tutaendelea kuwalaani.

Usitupangie cha kufanya. Mauti iwafunike
 
Hii
Padre Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), ametoa kauli nzito akisema kuwa viongozi wa dini lazima waonyeshe wazi kwamba aliyehusika katika mauaji ya Ally Mohamed Kibao amefanya kosa kubwa na ni laana kwa Mwenyezi Mungu.

Pia, Soma: Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Padre Kitima alisisitiza kuwa, "Aliyemuua Kibao amefanya kosa baya na ni laana kwa Mwenyezi Mungu. Kama viongozi wa dini, lazima tuseme hili. Tunalaani vikali vitendo vya uhalifu kama hivi."

Aliongeza, "Unafikiri watoto wa Mzee Kibao, aliyeuawa kinyama, wataonana vema na wale wanaohisiwa? Hii imejenga chuki kubwa kati ya familia na jamii. Tunapiga vita, tuna laani, na tunahitaji aliyemuua Kibao atubu kwa Mungu wake au achukuliwe hatua na sheria."

Padre Kitima alisisitiza kuwa, kama viongozi wa dini, ni jukumu lao kutoa ujumbe wa haki na amani, na kuonya dhidi ya vitendo vya kinyama vinavyovuruga jamii na kuleta machafuko.
Soma:
Hii ndo R.C bwana, cheza na mengine usicheze na kanisa hili , kweli yule mzee hapakuepo na sababu ya kumuua kinyama, bila kujali alikua mtumishi jeshini lakini je threat yake ilikua kubwa kiasi gani , katika nchi yenye wanajeshi , na vyombo vingine vya kiusalama?

Kuna kipindi nilileta mada isemayo Watekaji sio mda wataanza tiwa Adabu na Mungu. Nilielezea ndoto flani, na nikasema mengine nisingeweza yaweka katika andiko lile , Mungu yupo kazini
 
Ndiyo maana nasema ni huruma ya Mungu pekee ndio inaweza kumpatia ahuweni muuaji yeyeto yule na sio mbambamba nyinginezo 🐒
Unahaha sana ndugu.
Nyie endeleeni kuua huku mkiisogelea kwa kasi ghadhabu ya Muumba.

Msipotubu hakika kuzimu ina njaa nanyi
 
Padre Kitima yuko sahihi kabisa, mauaji hayo yamesababisha chuki kubwa sana kati ya Wananchi wa kawaida ambao ni wapenda haki dhidi ya Serikali na CCM, hususani kuibuka kwa chuki kati ya raia dhidi ya Jeshi la Polisi na TISS ambao kwenye mkasa huu wanashukiwa Moja kwa Moja kuhusika na mauaji hayo ya kinyama.


Kabisa Lina wajibu wa kukemea uovu mbaya kama huo.
Je, wewe binafsi ungejisikiaje endapo kama huyo mzee aliyeuawa kwenye mkasa huu angekuwa baba yako mzazi?
actually padre kitima anajaribu kujipambanua tu kwamba ana maslahi gani katika siasa Tanzania.

Infact,
hana ushawishi wala mashiko kwa kila anachoongea na waamini wa kanisa lake zaid ya kuwagawanya tu.

kulalamika hakuna maana yoyote na hakusaidii chochote.

sina hakika kama kifo humfurahisha yoyote gentleman, japo ulifurahi sana alipofariki hayati Magufuli 🐒
 
Unahaha sana ndugu.
Nyie endeleeni kuua huku mkiisogelea kwa kasi ghadhabu ya Muumba.

Msipotubu hakika kuzimu ina njaa nanyi
anae mbwelambwela ni Fr.Kitima na chadema gentleman🐒

kwani Muumba ni kaka yako ndio nibabaike na wewe.🤣

Mwenyezi Mungu ni wa wote wa mchao. Mshukuru Mungu kwa kila Jambo.
 
Endeleeni kuua na sisi Kanisa tutaendelea kuwalaani.

Usitupangie cha kufanya. Mauti iwafunike
Fr kitima tunamvumilia kumsikiliza ili tupate namna ya kumjibu na kumpuuza ingawa wengi wameanza kukwepa humilia zake za siasa za kulalamikia kila kitu bila kutoa suluhisho 🐒
 
Kanisa Katoliki kwa sasa ndiye msemaji pekee wa Wanyonge, ndugu zetu wa imani zingine tuungane na kanisa Katoliki kulaani ukatili unaoendelea kwa sasa nchini!
KANISA KATOLIKI LINAFANYA HAYO KIMKAKATI ZAIDI NA INAFAHAMIKA,WAPO KAZINI NA HUSUSANI MWAKANI NI MWAKA WA UCHAGUZI BASI WAMEONA NI BORA HARAKATI ZAO WAZIANZE MAPEMA ZAIDI.

WAPIGA MADILI TUH,NA NIA YAO INAFAHAMIKA.
 
..ahueni ipi??? Yuda iskariote alipata ahueni, au kwenda kuzimu kwako ndio ahueni! labda km ni hivyo uko sawa kulingana na unavyofahamu, lkn hiyo si ahueni! ahueni ni kuungama na kutubu kwa Mungu na kwa wanadamu hasa kwa familia ya Mzee Kibao!
Hiyo ni kulingana na Neema na Baraka za Mungu kwa mtu huyo gentleman.

unaungama nini sasa kama sio kuomba huruma ya Mungu? 🤣

au wewe huwa unaungama kwa nani na kusamehewa dhambi ya kuua?🤣

unaungama kwa wanadamu?🤣
 
Hiyo ni kulingana na Neema na Baraka za Mungu kwa mtu huyo gentleman.

unaungama nini sasa kama sio kuomba huruma ya Mungu? 🤣

au wewe huwa unaungama kwa nani na kusamehewa dhambi ya kuua?🤣

unaungama kwa wanadamu?🤣
Itakuwa ni sawa na kumuelimisha juha km unachokisema huwezi kutoa reference yoyote..sasa umetoka kwenye huruma ya Mungu umeenda kwenye Neema na Baraka ya Mungu..unafahamu hata maana ya maneno haya au unajitamkia tu..! soma kisa cha muuaji wa kwanza Kaini na vile Mungu alisema nae kwa habari ya kitendo alichofanya.
 
Kama kanisa inafaa kuiombea Neema na Baraka za Mungu familia ya Mzee Kibao..

Lakin zaid sana kumuombea huruma ya Mungu muuaji wa Mzee Kibao.

Mengine nadhani sio wajibu wa kanisa bali inaweza kua uchochezi zaidi 🐒
Itakuwa underwear yako imeshonewa na kitambaaa Cha bendera ya ccm sio bure ,huo uchochezi uko wap sasa😏😏😏😏
 
Back
Top Bottom