Ni aibu hii sio nchi aliyoiacha Mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa ni mwenyeji wa vikundi vingi vya wapigania uhuru na kutoa hifadhi ikiwepo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika. Miongoni mwa waliowahi kuishi Tanzania ni Nelson Mandela na Samora Machel.
“Nchi ambayo ilikuwa inakimbiliwa na kila mtu kuja kujifunza siasa safi, sasa hivi zipo nchi zinakuja kujifunza siasa chafu. Kuna nchi moja imejifunza juzi siasa zetu chafu tulizozifanya 2020, tunavyoongea hapa sasa hivi wanauana, walikuja wakajifunza hapa, na mwaka huu pia walikuja. Tuliwafundisha siasa safi wakawa wana uvumilivu lakini juzi tukawafundisha siasa chafu; namna ya kuwashughulikia wapinzani, wamewashughilikia wapinzani na hali ni mbaya kule”- Padre Dkt. Charles Kitima.
Leo ni tofauti wahuni wanaotaka kuharibu demokrasia za nchi zao, kujifunza kuiba kura na kupindua matokeo ya uchaguzi na kuweka vibaraka wao ndio tunaowakaribisha kuja kujifunza siasa chafu kutoka kwetu. Aibu.