Padre Dkt. Kitima: Zipo nchi siku hizi zinakuja kujifunza siasa chafu Tanzania

Ni aibu hii sio nchi aliyoiacha Mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa ni mwenyeji wa vikundi vingi vya wapigania uhuru na kutoa hifadhi ikiwepo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika. Miongoni mwa waliowahi kuishi Tanzania ni Nelson Mandela na Samora Machel.

“Nchi ambayo ilikuwa inakimbiliwa na kila mtu kuja kujifunza siasa safi, sasa hivi zipo nchi zinakuja kujifunza siasa chafu. Kuna nchi moja imejifunza juzi siasa zetu chafu tulizozifanya 2020, tunavyoongea hapa sasa hivi wanauana, walikuja wakajifunza hapa, na mwaka huu pia walikuja. Tuliwafundisha siasa safi wakawa wana uvumilivu lakini juzi tukawafundisha siasa chafu; namna ya kuwashughulikia wapinzani, wamewashughilikia wapinzani na hali ni mbaya kule”- Padre Dkt. Charles Kitima.

Leo ni tofauti wahuni wanaotaka kuharibu demokrasia za nchi zao, kujifunza kuiba kura na kupindua matokeo ya uchaguzi na kuweka vibaraka wao ndio tunaowakaribisha kuja kujifunza siasa chafu kutoka kwetu. Aibu.

Mwalimu Wangu (Mhadhiri Wangu) wa Media Law SAUT Mwanza mwaka 2008 na Vice Chancellor wangu Fr. Dkt. Charles Kitima akisema Kitu / Jambo Mimi Mwanafunzi wake GENTAMYCINE kamwe siwezi Kumpinga kwani najua yuko sahihi na nina uhakika nae kwa Mtazamo wake.
 
Padre Kitima huwa anachemka katika maoni yake mara nyingi tu.

Liberia walichinjana miaka ya nyuma na kwa sasa ni nchi imejaa vilema wanaotembea na magongo, na wao walikuja nchini kwetu kujifunza siasa za uhasama?.

Sudan na Somalia wanapigana kabla hata yeye hajajiunga seminary kusomea upadre, na wao wamejifunzia hapa Tanzania hizo siasa za chuki?.

Huyu ni meneja wa kampeni wa CHADEMA wa mwaka 2020, anajisahau na kuliingiza kanisa zima kwenye siasa za vyama vingi, halitendei haki kanisa na sisi waumini.
Kwahiyo unaona ni sawa hayo mambo yasikemewe kwasababu kuna nchi zina machafuko toka zamani.kabla ya kumuona padre anakosea ulitakiwa hajiulize hizo nchi zilifikaje fikaje uko.Padre yuko sahihi kukemea ili nasisi tusifike uko kama hizo nchi ulizotolea mfano.Tumia akili zako vizuri.
 
Nelson Mandela HAJAWAHI kuishi Tanzania, bali alipita tu kwa siku kadhaa lengo ni kuomba kutumia passport ya Tanzania akiwa kwenye ziara ya nchi mnalimbali akiomba misaada ya chama chake cha ANC na tawi alilolianzisha la kijeshi la Umkhonto we Sizwe. Tena alikuwa analala kwa Waziri mmoja hivi hadi akasahau viatu vyake. Mzee Kikwete alimpelekea viatu vyake wakati wa msiba wake!😄😄😄😄
Kwa ushahidi zaidi, soma kitabu chake alichoandika mwenyewe cha "The Long Walk to Freedom".
Nsilo Swai..1962 alipita hapa Tanzania......
 
Huyu padre abaki kwenye dini. Hajui siasa. Mawazo yake yameegemea kwenye mtazamo wa Chadema ambayo yeye pia ni mfuasi. Angewaambia wenzake wajifumze siasa za hoja sio za matukio.
Nikuulize kitu, siasa inatakiwa izungumzwe na nani?
Kitima ni mwananchi pia.
 
wanaacha kuhubiri dini wanataka kuwa wanasiasa ni ujinga wa hali ya juu hawa wanaojifanya watumnishi kumbe wanasiasa
Nenda kamsome Muhamad na vita alivyokuwa navyo. Usiwe mjinga dogo. Pata Elimu. Hawa watumishi wanaongoza watu. Mbona wanasiasa huenda kwa hawa hawa kuombewa? Na mbona wakisema Maza mitano tena mnawasifia? Wakisema amechaguliwa na mungus mnawakubalia?wakipinga uchafu ndo hawafai kwenye siasa?wawe wanaimba sifa na mapambio
 
Huu ni wakati muafaka wa kurudi na kutulia tukiomba Mwenyezi Mungu atuongoze salama. Padri Kitima, yes kusema ni muhimu, lakini lazima tuliombee sana Taifa letu.
Unajua fika, hakuna majawabu rahisi kwenye changamoto tunazopambana nazo
 
wanaacha kuhubiri dini wanataka kuwa wanasiasa ni ujinga wa hali ya juu hawa wanaojifanya watumnishi kumbe wanasiasa
Yule majaliwa juzi alienda pale mwalimu Nyerere kufanya nn na wale mashehe?ningekupa neno baya hadi ungechafukwa ila acha niache tu
 
Ni aibu hii sio nchi aliyoiacha Mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa ni mwenyeji wa vikundi vingi vya wapigania uhuru na kutoa hifadhi ikiwepo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika. Miongoni mwa waliowahi kuishi Tanzania ni Nelson Mandela na Samora Machel.

“Nchi ambayo ilikuwa inakimbiliwa na kila mtu kuja kujifunza siasa safi, sasa hivi zipo nchi zinakuja kujifunza siasa chafu. Kuna nchi moja imejifunza juzi siasa zetu chafu tulizozifanya 2020, tunavyoongea hapa sasa hivi wanauana, walikuja wakajifunza hapa, na mwaka huu pia walikuja. Tuliwafundisha siasa safi wakawa wana uvumilivu lakini juzi tukawafundisha siasa chafu; namna ya kuwashughulikia wapinzani, wamewashughilikia wapinzani na hali ni mbaya kule”- Padre Dkt. Charles Kitima.

Leo ni tofauti wahuni wanaotaka kuharibu demokrasia za nchi zao, kujifunza kuiba kura na kupindua matokeo ya uchaguzi na kuweka vibaraka wao ndio tunaowakaribisha kuja kujifunza siasa chafu kutoka kwetu. Aibu.

Tumuombee sana Padre Kitima, Mungu azidi kumlinda ili 'watesi' wasije wakamtumia mamluki ili kumuangamiza.
Ukiwa mtu unayesema Ukweli Sana, Mpigania haki, mpinga rushwa, ufisadi au mpinga dhuluma, badi tambua ya kwamba Afrika siyo sehemu salama wala siyo Mahali salama kwako kwa kuishi.
 
Ni aibu hii sio nchi aliyoiacha Mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa ni mwenyeji wa vikundi vingi vya wapigania uhuru na kutoa hifadhi ikiwepo Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika. Miongoni mwa waliowahi kuishi Tanzania ni Nelson Mandela na Samora Machel.

“Nchi ambayo ilikuwa inakimbiliwa na kila mtu kuja kujifunza siasa safi, sasa hivi zipo nchi zinakuja kujifunza siasa chafu. Kuna nchi moja imejifunza juzi siasa zetu chafu tulizozifanya 2020, tunavyoongea hapa sasa hivi wanauana, walikuja wakajifunza hapa, na mwaka huu pia walikuja. Tuliwafundisha siasa safi wakawa wana uvumilivu lakini juzi tukawafundisha siasa chafu; namna ya kuwashughulikia wapinzani, wamewashughilikia wapinzani na hali ni mbaya kule”- Padre Dkt. Charles Kitima.

Leo ni tofauti wahuni wanaotaka kuharibu demokrasia za nchi zao, kujifunza kuiba kura na kupindua matokeo ya uchaguzi na kuweka vibaraka wao ndio tunaowakaribisha kuja kujifunza siasa chafu kutoka kwetu. Aibu.

Pale kusini kwetu hapo labda. . . . . . . Eeh MUNGU ondosha madhila haya !
 
Huyu padre abaki kwenye dini. Hajui siasa. Mawazo yake yameegemea kwenye mtazamo wa Chadema ambayo yeye pia ni mfuasi. Angewaambia wenzake wajifumze siasa za hoja sio za matukio.
Ukiwa na ukinzani na ccm unakuwa chadema kumbe vyama vingine vyote ni ccm B?!.Nyie ndio mnaotufanya waafrika tuonekane tuko primitive.
 
Siasa za kipinzani ni zipi na zisizo za kipinzani ni zipi.
Anazozifanya huyo Padre wetu, siasa za kujifanya anatoa tu maoni ya kiungwana. Anakosoa hata masuala asiyo na utaalam nayo akidhani anao uelewa mpana na kibaya huwapata wengi wetu tusio na uelewa wa kina.
 
Kwahiyo unaona ni sawa hayo mambo yasikemewe kwasababu kuna nchi zina machafuko toka zamani.kabla ya kumuona padre anakosea ulitakiwa hajiulize hizo nchi zilifikaje fikaje uko.Padre yuko sahihi kukemea ili nasisi tusifike uko kama hizo nchi ulizotolea mfano.Tumia akili zako vizuri.
Akikemea asipokemea ukweli ni kwamba hana uwezo wa kubadilisha hali halisi.

Ndio maana nimesema zipo nchi zina vita miaka mingi kabla hata hajaenda seminari kusomea upadre hivyo maoni yake hayana chochote kipya.
 
Back
Top Bottom