GE2025 Padre Mwabena: Kanisa Katoliki linawahamasisha wananchi kupiga kura siku ikifika

GE2025 Padre Mwabena: Kanisa Katoliki linawahamasisha wananchi kupiga kura siku ikifika

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Paroko Msaidizi wa Parokia ya Peramiho, Padre Frederick Mwabena amesema ni wajibu wa Kanisa Katoliki kutunza amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Padre Mwabena amesisitiza kuwa Kanisa Katoliki linawahamasisha wananchi kupiga kura siku ikifika, kwani ni haki yao ya msingi.

Pia ametoa wito kwa waumini wa Kanisa Katoliki kutunza amani kuanzia kwa mtu mmoja mmoja na kwa wengine ilI kuepusha migongano isiyo ya lazima wakati wa uchaguzi.

Wananchi wakapige kura za nini wakati kila mtu aliye na akili timamu anajua nani atatangazwa mshindi?

Nchi imejaa majuha ya kutupwa kabisa.
 
Hata akihamasisha kwa kujigaragaza barabarani! Bado mimi kama mimi sitashiriki! Na uwezo wa kunipangia hana.
Wewe hata usiposhiriki wengine watashiriki na uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa.
 
Wananchi wakapige kura za nini wakati kila mtu aliye na akili timamu anajua nani atatangazwa mshindi?

Nchi imejaa majuha ya kutupwa kabisa.
Mshindi ni yule atakayepata kura nyingi.
 
Ambaye obviously ni mgombea wa CCM.

Hakuna sababu ya kupiga kura.
Kwa mazingira yeyote kwa sasa bado CCM ana numbers. Ni muhimu kuukubali ukweli mchungu..

Kuna maeneo mengi sana bado ni Green - yatampigia tu mgombea wa CCM. Toss up constituencies hazifiki hata 50. Ndiyo maana hata US - jimbo kama California lenye electoral votes 55 limekuwa likivote blue no matter mgombea wa Republican ni mzuri kiasi gani. Kusema watu hawatapiga kura ni kutokuelewa dhana ya demokrasia na electoral map ya Nchi yetu.

Ndiyo maana hata Padri Kitima alisema no matter what kwa sasa CCM ina ushindi wa zaidi ya 70%... Kanisa linajua na kama ni mfuatiliji unajua. Kuna scenes tu zinatengenezwa. Ila basi jamaa wana wafia dini wao. Kanda ya kati ni moja wapo; kanda ya pwani ni nyingine baada ya CUF kufa wameitek yote, mikoa ya kanda ya ziwa bado wanauungwaji mkono mkubwa sana kwenye majimbo ya vijijini... kanda y kaskazini ndiyo kuna toss up kidogo sana... sasa unategemea nn?
 
Kanda ipi ya Kaskazini kuna toss kidogo sana.?Jimbo lipi?Wacha wajipe moyo.Hakuna toss up yeyote Kanda ya Kaskazini ni CCM tupu.
 
Kanda ipi ya Kaskazini kuna toss kidogo sana.?Jimbo lipi?Wacha kujipa moyo.Hakuna toss up yeyote Kanda ya Kaskazini ni CCM tupu.
Karatu ni CDM, Babati ni toss up, Arusha Mjini ni toss up (na imelean CDM - hadi uwe na mgombea mgumu sana (sio kina Batlida), Hai ni CDM, Mbulu pia ni toss up (japo imelean CCM), Vunjo huwa haitabiriki. Moshi mjini baada ya Ndesa kuondoka imerudi CCM.... Mengine sawa ni CCM (na hapa nazungumzia Mkoa wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara). Kwa Tanga yote ni CCM.
 
Unaishi kwenye past.Hakuna toss up yeyote.Arusha Mjini ipo CCM, Karatu CCM,Moshi mjini mbunge ni Ibrahim Shayo,Vunjo ni Enock Koola.
Kilimanjaro kidogo wenye uhai kwenye udiwani ni Chaumma. Hasa Hai na Siha
 
Msimamo wa kanisa hauwezi kutolewa na mtu kama huyu..utaratibu wa Kanisa unajulikana!
 
Back
Top Bottom