Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Wana Jamii From!

Bila yakupoteza muda naomba kufahamu jambo moja zito ambalo kwa uelewa wangu nimeshindwa lipatia majibu!

Hivi inawezekana vipi Mtumishi wa Mungu Padre awe mwanajeshi tena komandoo??

Picha hapo chini ni Padre Henry,ambaye ni mwanajeshi komandoo,ambaye katunukiwa PhD yake ya Architecture!

Unamkumbuka Jaji Agustino Ramadhani?
Alikuwa Jaji(degree ya sheria),alikuwa mwanajeshi,na alisomea uchungaji,akawa padre wa Anglicans church.
Inawezekana sana.
Siku hizi kanisa katoriki,huwafata vijana waliopo vyuoni wanaosomea taaluma mbali mbali na kuwapa nafasi ya kuwa mapadre,unamaliza shahada yako ya uhandisi,ualimu,nk then unaenda kuwa padre!!!!
 
Kwa hiyo ?
Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!

Malisa GJ
View attachment 2033162
 
Basi, wapo wengi tu hata hawa mitume na manabii, wainjilisti, wachungaji na masheikh tuswachukulie poa ni watu wa kitengo wale. Ukizidi kuchunguza utakuta hata wanamuziki na wasanii wapo
Anajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.

IMG_2676.jpg

Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!

Credit @malisa_gj
 
Hongera zake...

Atakua ana sauti tatu...
Ya kufundishia, ya amri na ya kiuchungaji...
 
Anajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.
Yapu mbona anajulikana hivyo hata wa nchi pia hujulikana nothing new..
Usipojua ww wengine wajua
 
Back
Top Bottom