I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Movie zinawaharibu..
Huyo anajulikana siku zote, vijana msipende conspiracy theories
Anajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.Huyu Fr anajulikana sana, wewe umemjua leo kwa sababu kagraduate!
Unamkumbuka Jaji Agustino Ramadhani?Wana Jamii From!
Bila yakupoteza muda naomba kufahamu jambo moja zito ambalo kwa uelewa wangu nimeshindwa lipatia majibu!
Hivi inawezekana vipi Mtumishi wa Mungu Padre awe mwanajeshi tena komandoo??
Picha hapo chini ni Padre Henry,ambaye ni mwanajeshi komandoo,ambaye katunukiwa PhD yake ya Architecture!
Hakuna tofauti
Cv yake kijeshi amefika hadi cheo Cha Meja.Duh...
Ningependa kujua cv yake kijeshi
Kapigana vita gani
Ova
Sio chini ya 5Duh!,niongeze swali hapo hadi kupewa daraja la upadre ni miaka mingapi?
Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.
Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.
Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.
Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.
Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).
Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!
Malisa GJ
View attachment 2033162
Basi, wapo wengi tu hata hawa mitume na manabii, wainjilisti, wachungaji na masheikh tuswachukulie poa ni watu wa kitengo wale. Ukizidi kuchunguza utakuta hata wanamuziki na wasanii wapoAnajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.
Acha kuwa kama bi kidude mkuu!Uzi uunganishwe, Halafu ni Architect, sio Architecture, na ni chuo kikuu Ardhi, sio chuo kikuu cha Ardhi
Kwenye hio videoMambo ya black belt yapo wapi?
Exactly Apostles of JesusNa pia kwenye andiko naona wamekosea sio padri wa jimbo ni shirika.
Yapu mbona anajulikana hivyo hata wa nchi pia hujulikana nothing new..Anajulikana ndio sijakataa hata mimi namfahamu, lakini je, ni wote tulikuwa tunafahamu kuwa ni manajeshi komandoo? Point yangu ni ilikuwa hapo.
Pastor wa kwio? Fala huyo. Amekaa tu amebuni mbwinu ya kula pesa za wanawake na wamama akajipa na upastor. Mwulize amekuaje pastor. Watu waache shobo na makanisa ya watu.[emoji23][emoji23][emoji23]
Unamtukana Pastor?