Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Nambeni ufafanuzi anawezaje kufanya hayo yote ya Uanajeshi na Upadri?
Kiufupi huyo sio mwanajeshi, bali alihitajika kwenda South Sudan kwa ajili ya kutoa huduma ya kiroho, hivyo alipewa hadhi ili aendane na wale Machaplain wa kijeshi. Kwa Tanzania hio haiwezekani kwani hadi sasa haipo rasmi majeshini.
Na hata hao waliokuwa kina Augostino Ramadhan walianzia jeshini lakini baadae(kuacha/kustaafu) ndipo wakajiingiza kwenye upadri/uchungaji lakini sio kuwa wachungaji wakiwa jeshini.
Huyo jamaa sio komandoo pia ni kitu ambacho kwa nchi yetu hakiwezekani labda kama ni komandoo wa jeshi la wokovu.
Na kama angekuwa ni mwanajeshi kweli wa JWTZ kwanini asiweke army number yake?
 
Kapewa uanajeshi kama zawadi tu yeye alienda kule kama mchungaji tu
Kuna wale Machaplain, ambao huwa ni wanajeshi kitu ambacho kwenye jwtz hakipo rasmi, hivyo kuhitajika kwake kwenda kutoa huduma za kiroho kulisababisha apewe tu hadhi lakini yeye kachukulia serious! Nchi kama Afrika kusini ndio zinao hao Machaplain. [emoji1474]
 
Ngoja siku ziende, one day utasikia wamemwita akajieleze vizuri. Maana alichokifanya ni kuvunja sheria za nchi.
 
Kuna uwezekano akawa pia kwenye kundi la 'wasiojulikana'.
 
Ngoja siku ziende, one day utasikia wamemwita akajieleze vizuri. Maana alichokifanya ni kuvunja sheria za nchi.
Je, wanajeshi waliowahi ku-graduate kabla yake kwa ngazi ya elimu ya juu walivaaje?
 
Je, wanajeshi waliowahi ku-graduate walivaaje?
Ni kinyume na utaratibu kuchanganya mavazi ya kijeshi na mavazi mengine yoyote, ndio maana hata hao wanajeshi wanaograduate kama wamesomea uraiani watavaa mavazi ya kiraia, kama mafunzo hayo yalitolewa jeshini watavaa kijeshi ama kiraia kulingana na maelekezo yatakayotolewa. Lakini hawachanganyi mavazi.
 
Na ndio sheria inavyosema au hawakuwahi tu kufanya hivyo? Hivi nguo za ndani mfano vest, boxer, bra nazo ni za kijeshi?
 
Na ndio sheria inavyosema au hawakuwahi tu kufanya hivyo? Hivi nguo za ndani mfano vest, boxer, bra nazo ni za kijeshi?
Hapana, Namaanisha vazi linaloonekana nje, halitakiwi kuchanganywa na vazi jengine lolote la kiraia.
Mfano mzuri kwani aliyekuwa rais wa Tanzania awamu ya 4 si ni mwanajeshi? Je alipotunukiwa shahada yake ya uzamivu alivaa kijeshi?
Na wapo wengi tu wanajeshi waliotunukiwa shahada zao lakini wala huwezi kuwatambua kwasababu wala hawavai/hawatovaa mavazi ya kijeshi wakati wakitunukiwa.
 
Kwa nini anavaa sare za jeshi?
 
Yes kachukulia serious sana yaan mpaka leo anavaa magwanda nje ya nguo za kipadre
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…